Mwandishi Wetu, Kigoma Yetu
Wakulima Mkoani Kigoma wameishukuru halmashauri ya mji wa huo kwa kuwapatia matrekta matano na powertiller mbili ambazo ni chachu ya kuongeza kipato cha familia na kuinua kilimo kwanza Mkoani hapa.
Hafla ya uzinduzi wa nyenzo hizo za kisasa za kilimo zitawanufaisha wakazi wa vijiji vitano katika wilaya za Uvinza, Kigoma, mkigo, Mwamgongo na Lugufu uliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Khadija Nyemba.
Uzinduzi wa matrekta hayo ni kiashiria cha kuanza kwa kilimo cha kisasa na utekelezaji wa kilimo kwanza kwa lengo la kuwaondolea adha wakulima na kuepukana na kilimo cha jembe la mkono.
Mrisho Msolombogo mkulima wa kijiji cha Kidahwe anaishukuru serikali kwa kuwakumbuka na kwamba itawaongezea kasi ya uzalishaji na kipato chao cha familia.
Alisema kuwa awali walitumia sh.80,000 hadi sh.100,000 kuwalipa vibarua wa jembe la mkono lakini kuja kwa matrekta hayo na kuwekwa kwa bei ya chini ya sh.40.000 itawapunguzia gharama na kuharakisha uzalishaji katika kilimo.
Kwa upande wake Nezia Simon ambaye ni mkulima katika kijiji cha matendo alisema msaada huo utasaidia wanawake kuondokana na majukumu mengi majumban.
“Kupitia trekta itatusaidia wanawake kulea familia zetu kwa umakini zaidi kuliko ilivyokuwa katika kilimo cha jembe la mkono maana wengi huacha familia zetu katika mazingira tete, watoto wakiwa peke yao nyumbani hali ambayo ni hatari kwa ustawi wao.
Khadija Nyemba alipongeza halmashauri hiyo kwa kutimiza moja ya mikakati yake hasa mradi wa trekta ili kuwalimishia wakulima kwa kuchangia kiasi kidogo cha fedha
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment