Home » » WAZEE WALIA NA SERIKALI

WAZEE WALIA NA SERIKALI

Na Mwandishi Wetu, Kigoma.
ASASI isiyokuwa ya Kiserikali ya Saidia Wazee Tanzania (SAWATA) iliyopo Mkoani Kigoma, imeitaka Serikali kuwalinda wazee kiuchumi, pamoja na usalama wa maisha yao kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na Kaimu mwenyekiti wa SAWATA Mama Kokupima wakati akizungumza na wandishi wa Habari wilayani Kasulu Mkoa wa Kigoma, katika kaikao cha wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kuhusishwa na imani za kishirikina,hali inayohatarisha maisha.
Mama Kokupima Alisema kuwa, kwa tathimini waliyofanya waligundua wazee  wengi hubahatisha kupata chakula japo mlo mmoja kwa siku, hali inayowapelekea wazee hao kishi maisha muda mfupi, na kwamba hali hiyo inatokana na serikali kutoipa nguvu sera ya kuwasaidia wazee ikiwemo elimu ya kuendeleza vipaji vyao, malazi bora ili waishi maisha marefu yenye afya na furaha kama nchi za ulaya.
Alisema wazee wakiishi maisha mazuri kama ya wenzetu wa nx=chi za ulaya kwa upata mahitaji yote muhimu wataweza kuishi maisha malefu.
Kwa upande wake Ezekiel Lusambo aliyekuwa afisa elimu  ya watu wazima Kigoma mnamo 1974 alisema kuwa, kitabu kinachoanisha sera ya wazee kina dhima nzuri ingawa serikali haiichukulii umuhimu dhima hiyo, ikiwa yenyewe ndio chachu na mafuta ya mafanikio ya leo na kwamba serikali inapiga chenga kufanikisha sera hiyo kuwa sheria.
Lusambo alisema, serikali kupitia  wabunge waitumie sera hiyo kwa kuiwekewa sheria ili kuwanusuru wazee wa sasa na watarajiwa, kwani wengi wao hunyanyaswa kutokana na hali zao duni, huku wengi wakifukuzwa katika vijiji kwa tija ya ushirikina wakati wajane wakidhulumiwa haki zao za mirathi baada ya kufiwa na waume zao hali inayowalazimu kugeuka ombaomba ili kulea wajukuu zao.
Akifafanua  madhara yawapatayo wazee Emila Sethi alisema kuwa, katika wilaya ya Kasulu takribani kaya 10  za wazee wakiwemo wajane tayari zilichomwa moto kwa tija ya kuhusishwa na vitendo vya kishirikina ikiwa hakuna serikiali za mitaa hazijaweza bado  kuchukua hatua stahiki za kuweka ulinzi wa kutosha juu yao.
Aidha katika kikao hicho wazee kutambua kuwa wanahitajika katika jamii  na pia walielekezwa namna ya kuyafikisha mawazo yao siku ya kutoa maoni ya mchakato mzima wa uundwaji wa katiba mpya, pamoja na kutambua kuwa sera ya wazee iwekewe sheria na shurti ili kuboresha maisha tete ya wahanga hao.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa