Na
Diana Rubanguka, Kigoma Yetu
Wakazi
wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wako hatarini kupatwa na magonjwa ya mlipuko,
kutokana na wakazi wake kuweka vinyesi kwenye mifuko ya plastiki na
kuitupa mitaani kutokana na ukosefu wa vyoo.
Hayo
yamebainishwa leo kwenye Mdahalo wa Mazingira ambao umekasimiwa na Asasi
isiyokuwa ya Kiserikali ya Kigoma Un-Non Government Net-Work (KIUNGONET) ikiwa
na lengo la kuwakutanisha asasi za kiraia na watendaji wa serikali kujadili
changamoto ya uchafuzi wa mazingira ambayo imepelekea Manispaa ya kigoma Ujiji
kutunukiwa hati chafu kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo kwa miaka kumi huku
mkurugenzi wa manispaa hiyo akkikacha kuhudhuria mdahalo huo.
Kakozi
Abdallah mchangiaji alisema ,manispaa hiyo inakabiliwa na wakazi
wake kuendelea kutumia mifuko ya Rambo kwa kujisaidia haja kubwa na
hatimaye huitelekeza mitaani,hali inayochochea kutokea kwa magonjwa ya
milipuko ,
Abdallah
alidai kwamba, kutokana na hali tete ya uongozi wa halmashauri ya Kigoma ujiji
kushindwa kuwa na magari ya maji machafu pamoja na kushindwa kudhibiti jamii
husika na sheria ndogo ndogo ni chachu ya manispaa hiyo kushiriki kuchafua
mazingira kwa 60%.
Hellena
Geogre ni miongoni mwa wadau wa usafi wa mazingira alisema kuwa,jamii haina
elimu juu ya mabadiliko ya tabia nchi kuwa ni pamoja na utupaji wa taka
hovyo,hivyo kupitia midahalo ya asasi za kiraia wanachi waelimishwe ili
kudhibiti vitendo vya utupaji wa vinyesi holela.
“
ikiwa viongozi wa serikali hawataki kuja kwenye mdahalo kama huu wa kujadili
pamoja nini kifanyike na changamoto ya uchafunzi wa mazingira,watu wataendelea
kujisaidia ziwani na vinyesi vitatupwa sana tu,”alisema Mh,Diwani Kata ya
Buzebazeba Maftah.
Juma
Ramadhan Katibu Meza ya Duara alisema kuwa,tija iliyopo ni ushirikiano
kwa asasi zote za kiraia Kigoma kuhamasisha jamii kupitia mikutano na semina
kuwa jamii, ibadilike na tabia za uchafu, kwani mazingira safi ni pamoja
na afya njema.
Naye
Mkurugenzi wa KIUNGONET Costasine Mosha alisema kwamba,wenyeviti wa Serikali za
mitaa hawana elimu sahihi ya usafi wa mazingira na wajibu katika mitaa yao,hali
inayochangia jamii kujenga utamaduni wa kujisaidia ziwani badala ya
vyoo,wakidai “kujisaidia ziwani kuna raha yake”.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment