na Mwemezi Muhingo, Kibondo
MKAZI
wa Kijiji cha Kaziramihuda, Wilaya ya Kakonko, Mkoa wa Kigoma, Mohozya Joakimu
(25), ameuawa kwa kupigwa risasi huku wengine saba wakikimbilia kusikojulikana
baada ya kukutwa wakiiba mabati katika kikosi 824 cha Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) Kanembwa.
Taarifa
kutoka eneo la tukio zilisema kuwa, Joakimu akiwa na wenzake nane, walikutwa
juu ya paa la jengo moja wakiezua mabati ndani ya kikosi hicho, ndipo askari
waliokuwa doria waliwabaini na kupiga risasi iliyompata mtu huyo.
Tukio hilo
limetokea Novemba 19, mwaka huu, saa 6:00 usiku katika Kikosi cha 824 KJ,
Kanembwa, Wilaya mpya ya Kakonko.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Freiser Kashai, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kuwataka wananchi kuacha tabia za uharibifu wa mali za umma.
Eneo
hilo kabla ya kuchukuliwa na JKT lilikuwa likitumiwa kama kambi ya kuhifadhi
wakimbizi wa Burundi waliokimbia vita mwaka 1994.
0 comments:
Post a Comment