Na Mwandishi Wetu, Kigoma.
MWENYEKITI wa chama cha wananchi (CUF) Taifa Prof. Ibrahim Lipumba amemuomba Raisi Jakaya Mrisho Kikwete kutatua mgogoro wa ardhi kwa kusitisha zoezi la tathmini inayoendelea mkoani Kigoma kwa ajili ya ujenzi wa bandari kavu katika makazi wa wananchi.
Alisema hayo Jana(Juzi) wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Center katika Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji Mkoani hapa na kusema kuwa haki inatakiwa kupatikana kwa kila mwananchi na sio watu wachache kujinufaisha kupitia migogo ya wananchi hao.
Prof. Lipumba alisema kuwa ujenzi wa bandari hiyo ni muhimu kwa maslahi ya Taifa na wananchi ila ni lazima kujenga katika maeneo ambayo si makazi ya watu na hivyo kumuomba Raisi kulitilia mkazo suala hilo na kusitisha ujenzi huo ili kutaka haki ya wananchi wake.
" Hili ni jambo la ajabu viongozi wameng'ang'ania kujenga katika makazi ya watu sijui kunanini licha ya wananchi kuahidi kutoa mashamba pale watakapo lipwa fidia za mazao yao na kupisha ujenzi uendelee, kuna uwezekano baadhi ya viongozi wamesha jaza matumbo yao sasa wanataka wananchi wahame kwa lazima bila kujali kuwa ni makazi ya watu hii ni mipango ya kifisadi tu." alisema Prof. Lipumba.
Aidha Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalimu Seif Shariff Hamad aliwataka wananchi wa mkoa wa Kigoma kufanya mabadiliko ya dhati ambayo yataleta tija kwa Taifa na kuachana na vyama visivyo na dira na sera zisizo tekelezeka ambazo ni mashairi yalisi na tija.
"Kutokana na kuwa na sera zisizo tekelezeka katika nyanja mbalimbali hasa elimu ni lazima Taifa hili litakuwa la wajinga kutokana na kutowekeza katika sekta ya elimu, wanaomaliza shule ya msingi hawajui kusoma na kuandika huku watoto wa viongozi wakisoma nchi za nje ili viongozi waendelee kuwa ni wakurudhishana.alisema" Maalim Seif
hata katika mkutano huo Mwenyekiti wa chama hicho aliwakabidhi kadi wananchi thelethini walioamua kujiunga na chama hicho.
0 comments:
Post a Comment