Home » » WAFUNGWA GEREZA LA BANGWE WAJENGEWA MAJIKO BANIFU

WAFUNGWA GEREZA LA BANGWE WAJENGEWA MAJIKO BANIFU

Na, Mwandishi Wetu, Kigoma.
Mkuu  wa gereza la Bangwe lililopo manispaa ya Kigoma Ujiji, SSP Raphael Mwanyingili ameupongeza Mradi wa hifadhi wa Bonde la Ziwa Tanganyika kwa kuwajengea wafungwa majiko banifu ya kuni tatu ambayo hupunguza kasi ya ukataji wa miti kutokana na majiko hayo yanayobana matumizi ya kuni pamoja na kupunguza moshi ambao huathiri watumiaji wa nishati hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa mkoani hapo wakati wa mkutano wa kamati ya dharura iliyokuwa ikiwajibika kuboresha mapungufu ya makala ya Mradi wa hifadhi bonde la ziwa Tanganyika ambao ulifanywa na jopo la waandishi wa habari kutoka  kanda ya ziwa ikiwa na lengo la kuelezea utendaji kazi wa mradi huo pamoja na matokeo yake kwa vijiji tarajiwa sita ambavyo vimefanikiwa kupewa uwezo na mafunzo juu ya kulinda  vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira kutokana na matumizi ya jiko banifu.
Aidha SSP Raphael Mwanyingili alisema kuwa, mradi wa hifadhi bonde la ziwa Tanganyika imeonesha dhati ya kupunguza kero ya ukataji miti kwa kusudi la nishati ya moto katika vijiji teule ilagaga,kibondo,katavi,rukwa ,kasulu na kigoma pamoja na kuzisaidia tasisi za kiserikali likwemo gereza la bangwe  hali iliyopunguza matumizi ya kuni  nyingi kutoka tani qubiki 15 hadi tani 5 qubiki kwa mwezi.
 sisis tunakata kuni kutoka msitu wa kutengenezwa  tumeupanda upo karibu na gereza hatua kumi na tano tu, hili  gereza linahifadhi wafungwa  na mahabusu si chini ya 3,000 hivyo  kiasi cha kuni kinahitajika kwa wingi lakini kupitia mradi wa Bonde la ziwa Tanganyika imeisaidia serikali kupunguza fedha za kununua miche ya kurudishia miti ya m situ” alisema Mwanyingili.
Kwa upande wake Meneja mradi wa Bonde hilo Selebon Mushi, alisema kuwa dhamira ya mradi ni  kuwaweka wananchi katika  utayari  wa kupokea mabadiliko ya tabia nchi iwe fursa  kwa vijiji darasa wabadilishe kilimo cha kuhamahama ,tumbaku na matumizi ya mbolea kwa kufuga nyuki ambayo ina tija kwa familia zao na rafiki wa mazingira.
 Naye Leonard Nzilayilunde Afisa Mazingira Manispaa ya kigoma alisema kuwa, mradi umebaini manispaa ya kigoma ujiji kukosa eneo maalum la kutupa taka ngumu hali inayochochea wananchi kutupa taka holela na kusababisha uchafuzi wa ziwa hilo hali inayokwamishwa na miundombinu duni ya kuhifadhi taka hizo,huku akidai changamoto hiyo itakwisha mwaka huu baada ya kukamilika kwa ujenzi wa `Landfield ambapo taka hizo ambazo zitakuwa ajira kwa vijana pindi litakapokamilika.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa