Na Mwandishi Wetu,
Kigoma.
Mkurugenzi Mtendaji
Mamlaka ya Ziwa Tanganyika kutoka Burundi
Kaitira Katonda amekabidhi vitabu vya mpango mkakati wa
kulinda na kuhifadhi ziwa Tanganyika kwa mradi wa Programu
shirikishi ya Usimamizi wa ziwa Tanganyika kwa dhumuni la kuwafanya wadau wa
ziwa hilo kubaini mabadiliko ya tabia nchi kwa fursa ya kulinda na kuhifadhi
ziwa hilo.
Akikabidhi vitabu hivyo
Mbele ya Mkuu wa Wilaya ambaye ni mgeni lasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma Lt.Mstaafu Issa Machibya, alipokea vitabu hivyo kwa niaba
ya Lt.Machibya sambamba na fulana ,beji na kofia ambazo zina rangi
za nchi Nne ambazo ni Congo DRC Zambia, Tanzania na Burundi ikiwa na
hamasa ya uzalendo kwa viongozi husika ili iwe utambulisho wao pindi
wanapokuwa katika majukumu ya utekelezaji wa mradi .
Katonda alisema kuwa,
kutokana na changamoto ya ziwa hilo ambalo linatumiwa na nchi hizo, hawana budi
kuwaelimisha wananchi juu ya lengo la kuendeleza shughuli zao za
uvuvi,kilimo,hifadhi za wanyama na mimea, ili iwe chachu ya kuenzi ziwa hilo kwa
kizazi kijacho bila kuathiri viumbe hai waishio ndani ya ziwa hilo hali
itakayosaidia ziwa hilo kupungua kwa joto kutokana na changamoto ya ziwa
hilo kuongezeka kwa joto hali inayohatarisha uhai wa viumbe hai.
Kwa Upande wake mgeni
rasmi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya kwa niaba ya mkuu wa mkoa
Ramadhan Maneno alisema kuwa, amebaini tija ya kuzindua vitabu hivyo ambavyo ni
chachu kwa wananchi tegemezi wa mazao ya ziwa hilo kukubali mabadiliko
kulingana na karne ili ziwa liwe endelevu kwa jamii husika siku zijazo
huku akizitaka halmashauri za manispaa za mjini na wilayani kwa lengo la
kubaini ubadhirifu wa ziwa hilo kwa sheria na kanuni husika za mazingira.
“nazindua rasmi matumizi
ya hivi vitabu, beji, kofia na fulana hii ni tija kwa wahusika wawajibike
kulingana na hali halisi ya jamii yake lengo ziwa liwe salama na endelevu kwa
wajukuu zetu,bila kuisahau ofisi ya makamu wa raisi mazingira katika jitihada
zake za kuwainua wadau wenye kuelimisha wananchi juu ya mabadiliko ya nchi na
fursa kwa kuhifadhi na kulinda misitu,uoto wa asili kwa njia mbadala ya uvunaji
wa mazao ndani ya ziwa” alibainisha Maneno.
Naye Meneja Mradi Magese
Bulayi alitoa wito kwa asasi za kiraia ambao wanahitaji kushiriki kwenye
shughuli za uhifadhi wa mazingira wasisite kwenda kwenye mradi wao ili
wapatiwe malengo sita mtambukwa ya kuzingatia pindi wanapoelimisha wananchi ili
kuokoa uchafuzi wa mazingira ambayo ni chachu kwa kuathiri viumbe hai siku za
usoni.
0 comments:
Post a Comment