Na, Diana Rubanguka, Kigoma.
JESHI la Polisi Mkoani Kigoma limemfikisha mahakamani
Mathayo Ndolibihundo (30) Muha na Mkurima wa Nengo Wilayani Kibondo kujibu
shitaka la kukamatwa na Nyama ya Tembo kilo 15 zenye thamani ya zaidi ya 2m Tsh.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi
Mkoani Kigoma ACP Fraisser Kashai amesema kuwa mnamo 16 April 2013 majira ya
saa 9:45 katika kijiji cha Kabanga kilichopo Wilaya ya Kibondo mkoani humo,
askari polisi wakiwa doria walimkamta mtuhumiwa huyo na kumfikisha kituoni.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Mkoani humo linawashikilia
watu wawili Abasi Kalaheze (58) muha na mkulima wa kijiji cha Sogeeni kilichopo
wilayani Ksulu na Tashimililo Ejide
ambaye ni raia wa nchi jirani Burundi (Mhutu) (25) kwa tuhuma za kukamtwa na
miche ya Bhangi.
ACP Kashai alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na askari
polisi wakiwa kazini mnamo 17 April 2013 majira ya saa 12:00 katika kijiji cha
Sogeeni Tarafa ya Heru chini iliyopo wilayani Kasulu Mkoani Humo wakiwa
wamepanda miche 30 ya bhangi shambani kwa kuichanganya na tumbaku.
Aidha kashai alisema kuwa watuhumiwa wamefikishwa mahakani
leo ili kijibu mashitaka yanayowakabili, pia ametoa wito kwa wananchi kuendelea
kushirikiana na polisi ili kufichua uharifu na waharifu.
0 comments:
Post a Comment