Na Diana Rubanguka, Kigoma.
WATU wanne Mkoani
Kigoma wamekufa katika matukio tofauti likiwemo la watu wawili kusombwa
na mafuriko sambamba na kaya 200 wakati zaidi ya hekari 2000
kuharibiwa na mafuriko hayo yaliyotokea katika Kijiji cha Mgambazi eneo
la mwambao wa Ziwa Tanganyika katika Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma.
Akitoa taarifa
hiyo leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Frasser Kashai alisema kuwa
tukio la kwanza lilitokea Aprili 11 mwaka huu saa 9.usiku
ambapo chanzo cha mto huo kujaa ni mvua kubwa iliyonyesha milimani kwenye
kijiji cha mshamu mpakani na mpanda ambapo ulisababisha mto Mgambazi
uliopo katika Kijiji hicho kujaa na kusababisha madhara hayo kwa wananchi wa
eneo hilo.
Akiwataja
marehemu hao waliosobwa na mafuriko hayo Kamanda Kashai alisema ni Tabu Lubayi (25) na Nyamwelu
Rashid (22) wote wakazi wa Kijiji cha Mgambazi katika Wilaya ya Uvinza Mkoa wa
Kigoma ambapo tukio hilo lilitokana na mvua kubwa iliyonyesha kutwa nzima na
kusababisha mto Mgambazi kujaa maji na kuingia katika mashamba na nyumba za watu
hao.
Aidha Mwenyekiti
wa ulinzi na Usalama Mkuu wa Mkoa Kigoma Lt. Issa Machibya aliwataka
wakazi wa eneo hilo kuhama haraka iwezekanavyo ili kuepuka na madhara
mengine yanayoweza kujitokeza kwa kipindi hiki cha masika.
Katika tukio
hilo mwili wa mtu mmoja ulipatikana katika eneo la mtoni huku mwingine
kutoonekana hadi sasa na taratibu za kuutafuta zinaendelea ambapo taarifa
mbalimbali zinaeleza kuwa mafuriko kama hayo yalishawahi kutokea miaka mwaka
1999 na kusababisha madhara na kuziomba asasi mbalimbali zishiriki kuzisaidia
wahanga hao kimalazi,chakula na mavazi.
Katika tukio
lingine lililotokea aprili 14 mwaka huu, majira ya saa tisa usiku katika Kijiji
cha Kasuga Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma watu wasio julikana walivamia
nyumba ya mkazi mmoja na kufanya mauwaji pamoja na kujeruhi mtoto wa miaka
sita.
Kamanda Kashai
alimtaja bw. Nyamwelu Nesteli (30) ambaye alivamiwa na watu hao na kupigwa
risasi maeneo ya kifuani na kumsababishia kifo chake hapo papo pamoja na
kumjeruhi mtoto wa marehemu katika eneo la mkono wa kushoto ambaye alikuwa
amelala ndani.
Aidha katika tukio
lingine lililotokea Aprili 14 mwaka huu majira ya saa moja jioni katika eneo la
Reli Mpya Kata na Tarafa ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma Abel
Chikobela (65) aliuwawa kwa kupigwa na kitu kizito eneo la kichwani kutokana na
ugomvi wa kugombania miradhi.
Kamanda Kashai alimtaja aliyehusika na mauaji hayo kuwa ni
Ntauma Abel (31) mkulima na mkazi wa Nguruka alimuuwa ndugu yake kwa ajili ya
kugombania miradhi waliyoachiwa na wazazi wao, ambapo mtuhumiwa yupo chini ya
ulinzi wa polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi
kukamilika.
0 comments:
Post a Comment