Na Diana Rubanguka, Kigoma.
Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawasaka watu sita
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kwa tuhuma za kuvamia Shule ya Sekondari ya
kutwa ya Rungwe Mpya iliyopo wilaya ya Kasulu Mkoani humo.
Tukio hili lilotokea 21 April 2013 majira ya saa 01:00 usiku
limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma ACP Fraisser Kashai ambapo alisema kuwa watuhumiwa
hao walimfunga kamba Mlinzi wa Shule hiyo Obedi Muhindi (45) Mkazi wa Rungwe Mpya na kupora Solar Panel 05, Invetor
01, Simu tatu za mkononi, Laptop 01 pamoja na pesa taslim kiasi cha Tsh 45 elfu.
ACP Kashai alisema kuwa Majambazi hao
walipanda juu ya paa za madarasa na kuzingoa Solar hizo na kutokomea nazo.
Aidha alisema kuwa Majambazi hao walimkatakata Mlinzi huyo
kwa mapanga sehemu mbali mbali za mwili wake na amelazwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Kasulu kwa matibabu.
Hata hivyo alisema
kuwa kufuatia msako mkali uliofanyika kwa kushirikiana na wananchi Soral zote
zilizokuwa zimeporwa zilikutwa zimetelekezwa Porini na baada ya waharifu hao
kuwaona Polisi na wananchi wakiwafuatilia.
0 comments:
Post a Comment