Na Diana
Rubanguka, Kigoma
Idara ya Maafa Ofisi Ya Waziri Mkuu imetoa msaada wa vifaa
vya kujikimu kwa Wahanga wa
mafuriko yaliyotokea Aprili 11 katika kijiji cha Mgambazi kata ya Igalula
wilayani Kigoma.
Vifaa hivyo vimetolewa jana katika Kijiji hicho chini ya Mratibu wa maafa Mkoa wa Kigoma
bw. Rashid Maftaha ambapo amesema kuwa chanzo cha mafuriko hayo ni baada ya
mvua kali kunyesha na kusababisha Mto Mgambazi kujaa na hivyo kusababisha vifo vya watu wawili na zaidi ya
wakazi 500 kupoteza makazi yao.
Akikabidhi vifaa hivyo Mratibu huyo alisema kuwa vifaa hivyo vimegharama
kiasi cha jumla ya shilling
Milioni saba ikiwa ni pamoja na mahema, branket, sufuria na mafuta ya kupikia.
Kwa upande wake Kaimu
Mtendaji Kata ya Igalula Kijiji cha Mgambazi bw. Oscar Cosmas ametoa shukrani
na kuomba misaada hiyo iweze kuwa endelevu ili kuwanusuru wakazi hao.
Aidha tukio hilo la mafuriko katika kijiji hicho ni la mara
ya pili awali tukio hilo lilitokea mwaka 1999 ambapo kijiji hicho ni miongoni
mwa vijiji ambavyo vinakabiliwa na ukosefu wa mawasiliano na hivyo taarifa za
mafuriko kuchukua zaidi ya siku 5 kuifikia serikali ya mkoa wa Kigoma.
Hata hivyo wakazi wa kijiji hicho
wameiomba serikali kuweka mitambo itakayo wezesha mawasiliano kufuatia matatizo
hayoambayo yamekua yakiwakumba.
0 comments:
Post a Comment