BAADA ya serikali kupitia
wizara ya maliasili na utalii kujitangaza kwenye mipaka yake ya ndani na nje ya
Tanzania hatua hiyo imeanza kuonyesha mafanikio kutokana na ongezeko la idaidi
ya watalii wanaokuja nchini kwa ajili ya kutazama vivutio mbalimbali.
Miongoni mwa vivtutio
hivyo ni hifadhi za taifa, mapori tengefu, maporomoko ya asili, mila na
tamaduni za maisha ya waafrika na mlima Kilimanjaro ambavyo kwa pamoja
vimeifanya Tanzania kujulikana kimataifa.
Hifadhi ya Gombe ipo
umbali wa km 16 kaskazini mwa mji wa kigoma, katika fukwe za ziwa
Tanganyika Magharibi mwa Tanzania ambako anapatikana Sokwemtu mnyama mwenye
mila, desturi na tamaduni kama za binadamu ikiwemo kumiliki familia na kuwa na
ukoo.
Kama ilivyo kwa
binadamu sokwemtu ana uwezo wa kuishi zaidi ya miaka 50 hatua ambayo imekuwa
kivutio kwa watalii wa ndani na nje ya nchi kutumia pesa nyingi katika kusafiri
ili kujionea uhalisia huo.
Mhifadhi mkuu wa
hifadhi Bi. Noelia Myonga amesema fursa hiyo ya kutangaza maliasili na vivutio
imeiwezesha hifadhi ya taifa Gombe iliyopo mkoani Kigoma kuwa na ongezeko la
watalii kutoka 130 kwa mwaka 2008 hadi kufikia 2500 Juni mwaka huu.
Kabla ya kutangazwa
kuwa hifadhi ya taifa mwaka 1968, hifadhi ya taifa Gombe ilikuwa ni pori
tengefu ambalo lilitumiwa na mwingereza Jane Goodall kwa masuala ya utafiti wa
maisha ya Sokwemtu kupitia taasisi aliyoipa jina lake.
0 comments:
Post a Comment