HALMASHAURI ya
Manispaa ya Kigoma Ujiji huenda ikaingia kwenye kashfa na kushindwa kutekeleza
azma yake ya kujenga bandari mpya ya Gati la Kibirizi kufuatia wananchi
waliopisha ujenzi huo kulalamikia zoezi hilo kughubikwa na usiri mkubwa.
Zaidi ya
vibanda 800 vya biashara na nyumba za makazi vitabomolewa ili kupisha
ujenzi wa gati hilo unaojumuisha nchi tano zinazotumia ziwa Tanganyika lakini
wananchi wameanza kuonyesha hofu na woga katika hatua za awali za kufanyiwa
tathimini.
Wahanga wa eneo hilo
wamefika kwenye ofisi ya kata ya Kibirizi ambapo baadhi ya wananchi waliofika
baada ya kuitikia mwito wa viongozi wa Manispaa hiyo kupitia kwa mthamini
wake ili kujua nini kinaendelea.
Wananchi hao
wanapinga kitendo cha mthamini wa Manispaa hiyo Steven Ambrose kuwasainisha
fomu zisizokuwa na kiwango cha malipo ya pesa wanazostahili.
Usiri huu unawafanya
baadhi yao waamini kuwa huenda zoezi zima limeghubikwa na rushwa hali ambayo
inasababisha kugawanyika ambapo wengine wanakubali kusaini na wengine
wakitaa huku Afisa Mtendaji wa Kata ya Kibirizi Alfan Mofu akijaribu kutetea
uamuzi huo.
Hata hivyo mthamini
wa Manispaa hiyo Steven Ambrose ambaye alikuwa eneo la tukio hakuwa tayari
kulizungumzia suala hilo kwa madai kuwa yeye si msemaji.
0 comments:
Post a Comment