ZAHANATI
tatu za Misheni zilizopo Kata ya Kigoma Kaskazini Mkoani Kigoma zimekabidhiwa
Cheki ya Kiasi cha Tsh million 42 kwa lengo la kuwapatia huduma ya
kujifungua bure akina mama wajawazito ili kupunguza vifo
vitokanavyo na uzazi kwa kushindwa kugharamia huduma hiyo.
Fedha
hizo zimekabidhiwa jana Kalinzi Mkoani humo na Mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya kigoma vijijini, Bi. Miriam Mbaga kwa wawakilishi wa hospitali
ya Matyazo, Bugabiro na Kiganza ambazo zote zinamilikiwa na makanisa ikiwa ni
moja ya kampeni endelevu ya okoa maisha ya mama na mtoto ukanda wa kigoma
kaskazini na mwambao wa ziwa Tanganyika.
Akikabidhi
fedha hizo Mbaga aliwataka wanawake wa maeneo hayo wasiwe na hofu ya kufika
kwenye zahanati hizo pindi wanapohisi wakati wa kujifungua umekaribia na kwamba
serikali imesikia kilio chao cha gharama kubwa wanazopatiwa na hospitali hizo.
Aidha
akiwataka kina baba kutoongeza wake wengine kwa nafasi hyo badala
yake waongeze upendo kwa wake zao kwenye ujauzito kwa kuwasindikiza kliniki ili
kujua afya zao na kumlinda mtoto aliye tumboni.
Wakati
huo huo Mbaya aliwataka wahudumu wa hospitali hizo kuachana na tabia za
kuwanyanyasa wazazi pindi wawapo kwenye machungu ya kujifungua kwa kudai kuwa
wengi wao hawana uelewa wa kutosh ahivyo watumie njia mbadala ya kuwaelimisha.
“wahudumu
wa afya wa hospitali ya matyazo, bugabiro na kigaza tafadhali msiwanyanyase kwa
kuwatukana wakati wengi wao wanauwelewa mdogo na mkumbuke uchungu ni nusu ya
wazimu”. alisema Mbaga.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa wilaya Dkt. Edwin Kilimba
alisema kuwa, wananchi pamoja na wahudumu wa halmashauri watambue
jitihada za mkurugenzi wa sasa zina lengo la dhati kwa kina mama kufuatia vifo
ambavyo vimekua vikijitokeza katika wilaya yao.
Alisema
baadhi ya viongozi wa halmashauri kuwakingia vifua waganga katika vituo vya
afya vya serikali kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao kwa wagonjwa ni tatizo
linaleta utata katika kampeni ya okoa vifo vinavyoepukika kwa jamii husika.
Kwa
upande wa kina mama wa kata ya Kalinzi walisema kuwa tukio hilo ni la kipekee
tangu nchi ipate uhuru kwa kitendo cha mkurugenzi kuwa muwazi na mwenye lengo
kwa wanawake wa kigoma, huku wakidai kuwa kufuatia huduma hiyo kutolewa bure
hakuna mwanamke aliye tayari kuzalia nyumbani kwani uhakiaka wa huduma umewekwa
wazi.
0 comments:
Post a Comment