Emmanuel Ngowi akionyesha jenereta lisilotumia mafuta
Mkufunzi wa ufundi Stadi kutoka Mamlaka ya Mafunzo
ya Ufundi Stadi (Veta) Kigoma, Sirili Aloyce anasema kelele ni nyenzo
muhimu inayoweza kuzalisha nishati ya umeme.
Wakati baadhi ya watu wakitumia njia mbalimbali
kupambana na kelele za kila aina, wengine wanazitafuta ili waweze
kufanya shughuli mbalimbali zenye matokeo chanya kwenye maisha ya
binadamu.
Mkufunzi wa ufundi Stadi kutoka Mamlaka ya Mafunzo
ya Ufundi Stadi (Veta) Kigoma, Sirili Aloyce anasema kelele ni nyenzo
muhimu inayoweza kuzalisha nishati ya umeme.
Tayari Aloyce ameunda mashine inayotumia kelele na miyonzi ya mwanga kuzalisha nishati hiyo.
“Mashine hii hutumia kelele na mionzi ya mwanga
kuzalisha umeme. Imeundwa na betri ya volti 12 kama kianzishio kisha
huzalisha umeme wa volt 220 mpaka230. Umeme huo unaweza kuwasha balbu
10, televisheni na redio,” anasema Aloyce.
Akieleza jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi,
anasema imewekewa kinasa sauti (microphone) kinachopokea kelele zozote
zile na kuzipeleka kwenye mitambo ya kuikuza kabla ya kuchanganyika na
mionzi inayovutwa na kifaa maalum kisha kuchanganyika pamoja na kuchaji
betri.
“Sauti na mionzi inayokusanywa wakati mashine
imewashwa hukuzwa na kuingizwa kwenye mitambo ambayo hubadilishwa kuwa
umeme,” anasema.
Aloyce anayesema kuwa, yeye ndiye mgunduzi wa
teknolojia hiyo, anabainisha kuwa lengo lengo lake ni kuhakikisha kila
mwananchi anaweza kupata nishati hiyo kwa njia rahisi.
Hata hivyo anasema bado anaendelea na utafiti wake ili mashine hiyo izalishe umeme mkubwa zaidi.
“Nia yangu ni kuhakikisha kuwa umeme huu unasaidia watu nyumbani na matumizi ya viwandani,” anasema na kuongeza:
“Hadi sasa nimetumia Sh800,000 kuunda mashine hii,
hatua iliyobaki ya kuhakikisha inazalisha umeme mkubwa zaidi.
Haitachukua muda mrefu kwa sababu kazi iliyobaki siyo kubwa sana. Lengo
langu ni kuifanya izalishe umeme wa wati 6000 na kuifanya kuwa ya kisasa
zaidi.”
Jenereta ya kuzalisha umeme bila kutumia mafuta
Mbali na teknolojia hiyo ya kuzalisha umeme kwa
kutumia mawimbi ya sauti mbalimbali, mwanafunzi wa chuo hicho naye
ametegeneza jenereta inayoweza kuzalisha umeme bila kutumia mafuta.
CHANZO MWANANCHI GAZETI
0 comments:
Post a Comment