MHASIBU wa kampuni ya
pamba ameuawa kwa kupigwa risasi kichwani na kisha kuporwa zaidi ya shilingi
milioni nane wilayani Igunga.
Kamanda wa Polisi
Mkoani Tabora kamishna msaidizi wa Polisi Peter Ouma, alisema tukio hilo
limetokea Wilayani Igunga usiku wa kuamkia jana na kumtaja marehemu kuwa ni
Agnes Aron (44) aliyegiwa risasi ya kichwani na watu wanaodhaniwa ni majambazi
waliovamia kwenye ghala la pamba alilokuwepo.
Akizungumzia tukio
hilo, Kamanda Ouma amesema watu watatu walivamia ghala la pamba katika kijiji
cha Iyogelo,kata ya kining'inila,wilayani igunga majira ya saa mbili usiku na
kumpiga risasi kichwani mhasibu huyo kwa kutumia gobole.
Baada ya kumuua
walimpekua na kuchukua kiasi ambacho inakisiwa ni zaidi ya shilingi Milioni
nane alizokuwa nazo mhasibu huyo ndani ya ghala hilo.
Ameeleza kuwa mhasibu
huyo na wenzake walikuwa ndani ya ghala wakipokea pamba na kupakia kwenye
malori na ndipo walipovamiwa.
Hata hivyo amesema
tayari polisi inamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kuhusiana
na tukio hilo huku akitoa wito kwa makampuni ya pamba kutumia walinzi katika
shughuli zao.
kamanda Ouma
aliongeza kuwa atakuwa na mazungumzo na makampuni ya pamba ili kuwasisitiza
umuhimu wa kuwa na ulinzi katika shughuli zao huku akionya kutotembea na pesa
nyingi hadi usiku.
0 comments:
Post a Comment