UCHAGUZI wa Makamu Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma na wenyeviti wa kamati
mbalimbali za baraza la madiwani wa halmashauri hiyo nusra uvunjike baada ya
kutawaliwa na hisia za vyama kati ya Chama cha Mapinduzi CCM na NCCR Mageuzi.
Mvutano huo ulitokana
na kulingana kwa idadi ya wajumbe kati ya vyama vyote viwili huku chama cha
Wananchi CUF chenye diwani mmoja wa viti maalumu kikiwa kivutio ambapo kura
yake ilitakiwa na kila chama ili kishinde na hatimaye NCCR Mageuzi kiliibuka na
ushindi wa kura 21 dhidi ya kura 20 za CCM.
Hatua iliyolalamikiwa
na baadhi ya madiwani ni kitendo cha Mwenyekiti wa halmashauri ambaye anatoka
CCM kuketi kitako na timu ya wataalamu akiwemo Mkurugenzi Mtendaji ili
kuwapangia kamati wajumbe bila ridhaa yao hatua ambayo iliwakasirisha na
kupinga uamuzi huo.
Kikao hicho kutawaliwa
na hisia za kivyama kulisababisha ajenda nyingine kuchelewa kujadiliwa huku
wengine wakirushiana maneno ya kuwalaumu wabunge kuwa wazungumzaji kuliko
madiwani.
Wilaya ya Kasulu
kabla ya kugawanywa na kupatikana kwa wilaya mpya ya Buhigwe ilikuwa na majimbo
mawili ya uchaguzi yanayoongozwa na wabunge Agripina Buyogera na Moses Machali
wote kutoka chama NCCR Mageuzi huku huku diwani wa Kata ya Kasulu mjini
akiiongzea nguvu baada ya kuibuka mshindi katika nafasi ya makamu mwenyekiti wa
halmashauri hiyo.
0 comments:
Post a Comment