Home » » Mkandarasi ashindwa kukabidhi mradi

Mkandarasi ashindwa kukabidhi mradi



Na Diana Rubanguka, Kigoma.
MKANDARASI wa kampuni ya ILAGA JONTA iliyopo mkoani Kigoma ameshindwa kukabidhi mradi wa soko la Mgaraganza lililopo katika Kijiji cha Mgaraganza Mkoani humo kutokana na ujenzi wa soko hilo kuwa chini ya kiwango.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kijiji hicho Mwenyekiti wa Kijiji bw Yunusi Shabani alisema kuwa mkandarasi huyo ambaye alianza ujenzi wa soko hilo tangu Mai, 2010 na kutakiwa kukabidhi Septemba, 2010 ambapo ameshindwa kufanya hivyo kutokana na soko hilo kuto kuwa na ubora unaotakiwa. 
Bw. Shabani alisema kuwa ujenzi huo umechukua taakribani miaka miwili kutokana wakaguzi kutokuridhishwa na ujenzi huo ambao upo chini ya viwango na hivyo mkandarasi huyo kulazimika kufanya ukarabati wa mara kwa mara katika sokohilo.

Aidha mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 28 ambao upo chini ya serikali kupitia Dasp pamoja na nguvu za wananchi wa kijiji hicho bado haujakabidhiwa kwa wananchi kutokana na mapungufu hayo jambo ambalo limekuwa kero kwa wananchi wa kijiji hicho na kuitaka serikali kumchukulia hatua za kisheria kwa mkandarasi huyo kutokana na kukiuka mkataba wake.

Hata hivyo juhudi za kuwasiliana na mkandarasi zinaendelea ili kujua ni lini atakabidhi mradi huo kwa wananchi ili waweze kunufaika na mradi huo ambao wamechangia nguvu zao kwa asilimia 20 katika kuhakikisha mradi wa soko hilo unakamilika kwa wakati uliopangwa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa