Home » » INASIKITISHA SANA!KANG'ATWA USO NA BOSI WAKE NA KUWA KAMA KIUMBE CHA AJABU

INASIKITISHA SANA!KANG'ATWA USO NA BOSI WAKE NA KUWA KAMA KIUMBE CHA AJABU



KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo katika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Susuluka (16) anadaiwa kujeruhiwa vibaya usoni na bosi wake, Imani Paulo (36) kwa kung’atwa ng’atwa usoni na kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje, kama ambavyo anaonekana pichani.
Tukio hilo ambalo tunaweza kulifananisha na dunia kuelekea kufika mwisho, limegusa hisia za watu wengi hasa wakazi wa Kibondo, huku wengine wakitokwa na machozi kutokana na kuguswa na ukatili ambao amefanyiwa kijana huyo.Tunaweza kufikiria kuwa tukio hilo ni sinema, lakini Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamotto, ameliambia Majira kuwa tukio hilo limetokea miezi miwili iliyopita.
Akizungumza na Majira katika mahojiano maalumu, Mwamotto, alisema kuwa kabla ya kijana huyo kujeruhiwa na bosi wake, alimtuma dukani ili akamnunulie soda.Aliliambia Majirakuwa baada ya kufika nyumbani alimkuta bosi wake akiwa amemkaba koo mbwa na kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata mbwa huyo, alianza kuhema akitoa ulimi nje.
DC Mwamotto alisema kuwa mtuhumiwa huyo ghafla alianza kuung’ata ulimi wa mbwa na kisha kumeza vipande jambo lililosababisha mbwa huyo kupiga kelele kutokana na maumivu.Aliongeza kuwa aliendelea kula vipande vya ulimi huo wa mbwa hadi alipoumaliza.
“Unaweza kusema kuwa ni uongo, lakini ni tukio la kweli kabisa kwani mshtakiwa huyo aliendelea kula ulimi wote wa mbwa, huku kijana huyo akiendelea kumshangaa bosi wake kutokana na kitendo hicho kilichosababisha mbwa huyo kufa,”Wakati akiendelea kumshangaa bosi wake ghafla alimrukia na kumkamata kwa nguvu na kuanza kumng’ata kama mtu anayetafuna hindi la kuchoma.
“Mshtakiwa huyo alianza kumtafuna jicho moja na kufuatia jicho la pili na kisha kumeza vipande vya macho huku akiendelea kumshika kwa nguvu,” alisema DC Mwamotto wakati wa mahojiano naMajira.
Baada ya kumaliza kitendo hicho alisema kuwa mshtakiwa huyo alianza kumng’ata pua na kisha kumeza na vipande.
Alisema kuwa wakati anaendelea na kitendo hicho majeruhi huyo alikuwa akipiga kelele za kuomba msaada, lakini mshtakiwa huyo alianza kumng’ata tena kipande cha mdomo wa chini na kisha kusababisha meno kubaki nje.“Kutokana na kelele hizo wananchi waliamua kusogea karibu, lakini walikuta tayari, Susuluka amejeruhiwa vibaya usoni huku damu zikimtoka kwa wingi,” alisema.
Mwamotto alisema kuwa kutokana na hali hiyo wananchi walimvamia na kumpiga na kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Kibondo na majeruhi walimkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Kibondo.
Majira iliendelea na mahojiano hayo ambapo, mshtakiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya na kufunguliwa mashtaka ya kudhulu mwili.“Hivi sasa mshtakiwa yupo katika Gereza la Nyamisivi Kibondo, lakini cha kusikitisha tena akiwa huko alimng’ata na kula vipande vya nyama vya mguu mshtakiwa mwenzake,” alisema.
Alisema kuwa mshtakiwa mwenzake alimjeruhi vibaya na kupelekwa hospitalini hali iliyosababisha mshtakiwa huyo kutengwa na washtakiwa wenzake.“Mimi nimelazimika kwenda hadi gerezani na kufanya mahojiano na mshtakiwa huyu, kwani hili tukio linasikitisha sana lakini cha ajabu alitaka kufahamu je ameshtakiwa kwa makosa gani ya kuua mbwa au kumng’ata mtu,” alisema.
Alisema kuwa pia amelazimika kwenda kumjulia hali majeruhi huyo ambapo madaktari katika hospitali hiyo walishindwa kumtibia.“Nimeomba msaada kutoka Wizara ya Afya ili mgonjwa 
huyu akatibiwe India na tayari maandalizi yameanza kufanyika kwa kushirikiana na Hospitali ya Kibondo,” alisema.
Mwamotto alisema kuwa mgonjwa huyo hana pua, macho yamefumba, mdomo kwa kujeruhiwa vibaya usoni hali ambayo anahitaji matibabu zaidi.Amewaomba Watanzania kumsaidia kijana huyo ili aweze kwenda kutibiwa haraka nje pamoja na kupata msaada mbalimbali kwa kuwasiliana na mganga mkuu wa hospitali ya Kibondo ama kuwasiliana na Mhariri mtendaji wa gazeti laMajira
Habari hii kwa hisani ya gazeti la majira

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa