Home » » NGELEJA:KUNA UPOTOSHAJI DHIDI YA WARIOBA

NGELEJA:KUNA UPOTOSHAJI DHIDI YA WARIOBA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,William Ngeleja.
 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, William Ngeleja, amesema kuna upotoshaji unaofanywa kwa lengo la kuwafitinisha wajumbe wanaounga mkono muundo wa Muungano wa serikali tatu na Jaji Joseph Warioba aliyeongoza tume ya kuratibu maoni ya wananchi.
Ngeleja alisema hayo wakati akichangia mjadala wa Rasimu ya Katiba mpya, sura ya kwanza na ya sita bungeni jana.

Alisema wanachofanya wajumbe hao ni kuchambua na kueleza mapungufu yaliyomo kwenye Rasimu iliyopendekezwa kwa lengo la kuiboresha ili Katiba itakayoundwa iwe bora yenye kubeba maslahi ya wananchi badala ya kundi la watu wachache.

“Hakuna mtu anayeichukia Tume ya Warioba msitufitinishe, wananchi watuelewe tunapojadiliana hapa tunataka kutengeneza mustakabali wa taifa letu kwa siku nyingi zijazo” alisema.

Ngeleja alikosoa takwimu ziliopo kwenye Rasimu ya Katiba kuhusu idadi ya watu waliotoa maoni ya kutaka muundo wa serikali tatu kuwa haiwakilishi maoni halisi ya wananchi.

“Watu 17, 000 waliotoa maoni ya kutaka muundo wa serikali tatu ni asilimia mbili tu ya watu waliozungumzia muundo wa Muungano.

Wachambuzi wanasema angalau ingefikia asilia 30 ingekuwa na uhalali…wananchi, viongozi wa dini wa madehebu yote tujiulize ni sawa kuwaachia asilimia mbili kutuamualia hatma ya taifa letu?” alihoji Ngeleja.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa