Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKATI akiendelea na Kampeni ya ‘Rudisheni Pesa Zetu’, inayoshika
kasi mkoani Kigoma, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), Thomas
Kafulila, ametangaza kuanza kwa michuano ya kuwania ng’ombe sita
itakayoshirikisha timu za kata zinazounda jimbo hilo.
Akizungumza katika Kijiji cha Basanza, Kata ya Uvinza kwenye
mfululizo wa mikutano yake ya kampeni hiyo, Kafulila alizitaja kata
zitakazoshiriki michuano hiyo kuwa ni Uvinza, Nguruka, Sigunga,
Ilagala, Simbo, Sunuka, Kazuramimba, Kalya, Bulungu, Igalula, Mtego wa
Noti, Kandaga, Itebula na Mganza.
Alibainisha kuwa kila timu katika michuano hiyo itapewa jezi na
mpira, ili kujiandaa ambapo bingwa atajinyakulia zawadi ya ng’ombe
watatu, wakati mshindi wa pili akibeba ng’ombe wawili na mshindi wa
tatu akitoka na ng’ombe mmoja.
Aliwataka wachezaji wa timu shiriki kukubali matokeo katika michuano
hiyo, kwani kufunga na kufungwa ni kitu cha kawaida katika soka, kama
ilivyoonekana kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil, ambako
wenyeji licha ya ubora na umwamba wao duniani, walikubali kipigo cha
mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani.
Kafulila alisema kuwa lengo la michuano hiyo ni kuhamasisha meandeleo
ya michezo katika jimbo hilo, huku akijipanga kuratibu pia michuano ya
soka la wanawake
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment