Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JESHI la Polisi mkoani hapa, linawashikilia Elias Balandese na
Faustine Fidel kwa tuhuma za mauaji ya askari mgambo, Shabani Mbadi
mkazi wa Kijiji cha Nyamidaho wilayani Kasulu kwa kumchoma na kitu
chenye ncha kali upande wa kushoto wa kifua chake.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai, alisema Mbadi alijeruhiwa Julai 24
mwaka huu majira ya saa nne usiku wakati wakinywa pombe za kienyeji
pamoja na watuhumiwa.
Kashai, alisema kuwa Balandese ambaye ni raia wa Burundi, aliamua
kulipiza kisasi kwa kumuua askari mgambo huyo kutokana na kumkamata
katika zoezi la Oparesheni Kimbunga na kumfikisha kituo cha polisi kwa
kuwa alikuwa akiishi nchini kinyume na taratibu za nchi.
“Mauaji ya Shabani Mabadi yamefanyika kama kulipiza kisasi, kwani
wakati wa zoezi la Oparesheni Kimbunga marehemu aliwahi kumkamata
mtuhumiwa Elias Balandese kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali na
kumfikisha katika kituo cha polisi,” alisema Kashai.
Alisema Mbadi alipatwa na mauti wakati akiwa hospitali ya Wilaya ya
Kasulu akipatiwa matibabu, kutokana na majeraha aliyokuwa ameyapata.
Wakati huo huo, mtu mmoja amefariki dunia katika Manispaa ya Kigoma
Ujiji baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na kumfunga kamba,
miguuni, mikononi na kumfunga kitambaa mdomoni, hali iliyomsababishia
kukosa hewa na kufariki dunia
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment