Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA cha Alliance Transparency For Change
(ACT) Mkoa wa Kigoma, kimeahidi kumlinda na kumtetea Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), kutokana na changamoto
zinazomkumba kupitia watu wachache wanaotaka kumwangusha kisiasa.
Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya chama hicho,
Bw. Jaffar Kasisiko, aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Viwanja vya Cine Atlas, kwenye Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Alisema chama hicho hakipo tayari kuyafumbia
macho matatizo yanayomkuta Bw. Kabwe na kumshauri mbunge huyo aachane
na CHADEMA badala yake ajiunge na ACT ili aweze kukusanya wanachama
kuanzia ngazi ya kitongoji, vijiji, kata na wilaya.
Aliongeza kuwa, uongozi wa CHADEMA una hila
ya kusambaza maneno kwa umma dhidi ya Bw. Kabwe ili kulinda masilahi yao
binafsi badala ya kutetea haki za wanyonge.
“Kabwe asipoteze muda wa kulumbana na
uongozi wa CHADEMA, huu ni wakati mwafaka kwake kufanya uamuzi makini wa
kwenda kuifuta kesi dhidi ya chama chake mahakamani na kujiunga na
ACT,” alisema Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, Msafiri Wamalwa.
Katibu Mwenezi Wilaya ya Kigoma kutoka chama
hicho, Anzoluni Kibela, alisema ACT imeandaa kadi kwa ajili ya Bw.
Kabwe ambapo kuna wabunge 18 wapo tayari kujiunga na chama hicho kwenye
uzinduzi rasmi ulipangwa kufanyika mwanzoni mwa Septemba mwaka huu.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa,
Bw. Shaban Mambo, aliwasihi wananchi wamuunge mkono Bw. Kabwe
atakapojiunga na chama hicho ili aboreshe hali ya usafiri wa reli ya
kati kwa kuwaletea treni inayotumia umeme kwa gharama zake.
Baadhi ya wanachama wapya wa ACT akiwemo
aliyekuwa Mweka Hazina wa CHADEMA Kigoma Ujiji, Bw. Hamidu Hamis na
Katibu wa ACT wilayani humo, Bw. Haji Idd, walisema wamejiunga na chama
hicho ili kuleta uwazi uwajibikaji
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment