Home » » MBARONI KWA UVUVI HARAMU

MBARONI KWA UVUVI HARAMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

JESHI la Polisi mkoani Kigoma, linawashikilia watu watano wakiwemo raia wa Burundi kwa tuhuma za uvuvi haramu katika Ziwa Tanganyika eneo la kijiji cha Kiziba Wilaya ya Kigoma Vijijini, baada ya kuwakuta wakivua samaki kwa kutumia nyavu za sumu.
Akieleza tukio hilo ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Japhari Muhamed alisema kuwa polisi waliokuwa doria majini saa 5 hadi 7 usiku, waliwakuta wavuvi hao wakivua kwa kutumia nyavu hizo.
Aliwataja kuwa ni Ndikuri Sadock (30), Ruhitamo Johnclaud (17) wote wakiwa ni Wahutu wakazi wa Magala nchini Burundi na Idd Mussa (32), Athumani Ahamad (21) na Rashid Biziamo (17) wote wakiwa ni wakazi wa kijiji cha Mwamgongo.
“Nyavu walizokuwa wakizitumia zimeshakatazwa kisheria, kwanza nyavu zina matundu madogo chini ya nchi tatu, kitaalamu zinaitwa Monofilament, pia zilikuwa zimewekewa sumu ambayo samaki wakiingia katika vyavu hizo zinawaathiri na kufa haraka,” alisema Kamanda.
Aliongeza kuwa kasoro ya nyavu hizo zinaweza kukaa miaka 100 bila kuoza, kwa hiyo ikitokea bahati mbaya zikapotea ziwani, samaki wanaweza kuendelea kunasa na kufa hadi kuisha.
“Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa asili ya uvuvi huo ni nchini Burundi, sasa inaonekana kwa upande wao samaki wamepungua na sasa wanaelekea kwetu,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa