Kufuatia
ongezeko la baadhi ya wanaume wanaozitelekeza familia zao kwa
kisingizio cha maisha magumu chama cha waandishi wa habari wanawake
nchini- TAMWA kimelaani vitendo hivyo na kubaini njia pekee ya kutatua
tatizo hilo ni vyombo husika kuwachukulia sheria kali ili iwe fundisho
ambpo kumekuwa na ongezeko kubwa la wanawake wanaojitokeza mara baada ya
kutelekezwa na kuishi maisha ya kutegemea kusaidiwa kwa kuomba msaada
kwa watu binafsi na katika vyombo vya habari.
ITV imezungumza na Bi Judidhi Jumanne mkazi wa Singida
aliyetelekezwa na mume wake akiwa na ujauzito waa mienzi minne baada ya
kuishi nae kwa muda mrefu ambapo kwa uchungu amesema mara baada ya
kutelekezwa alilazimika kulea ujauzito huo peke yake bila kujua mwanaume
alikotokomea nana kubaini maisha anayoishi ya kusaidiwa na majirani
mara baada ya kuijifungua kwa oparesheni huku mtoto akiwa na tatizo la
kukosa tundu la kujisaidia haja kubwa na hivyo kutobolewa ubavuni.
Baadhi ya majirani waliobeba jukumu la kumsaidia binti huyo
wameendelea kulaani vikali vitendo hivyo na kuviita vya kinyama huku
wakiiomba vyomba husika kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe
fundisho.
Mkurugenzi mtendaji chama cha waandishi wa habari wanawake nchini
TAMWA Bi Valeria Msoka amekiri ongezeko kubwa la matatizo ya wanawake
kuendelea kutelekezwa kutokana na wengi kutokujua haki zao za msingi na
kutoa wito kwa mashirika,taasisi na vyombo vya dola kushirikiana ili
kuwachukulia sheria kali wale wote wanaobainika kufanya hivyo.
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment