Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Jafari Mohamed.
Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Kala, kilichopo mkoani Rukwa wakati meli hiyo ikitokea Mpulungu, Zambia kuelekea Burundi.
Mwakilishi wa meli hiyo mkoani Kigoma, Juliana Zakenda, alisema meli hiyo ilikuwa imebeba wafanyakazi 14 na tani 437 za mahindi.
Alisema kati ya wafanyakazi hao, ni mmoja tu alieokolewa huku hali yake ikiwa mbaya.
Alisema mtu huyo ni mfanyakazi wa meli hiyo na alijulikana kwa jina moja la Sefu na kwamba wafanyakazi wengine 13 hawajaopolewa.
Meneja wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Kigoma, Athumani Malibamba, alisema meli hiyo bado imezama na juhudi za kuitafuta zinaendelea.
Aliomba serikali kuweka vituo vya mawasiliano katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa Ziwa ili linapotokea tatizo kama hilo iwe rahisi kupata msaada na kwamba karibu vijiji vyote vinavyolizunguka ziwa hilo havina mawasiliano.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Jafari Mohamed, alithibitisha kitokea kwa tukio hilo na kwamba Polisi wanaendelea kuitafuta meli hiyo.
CHANZO:
NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment