Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge Mteule wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.
Mbunge Mteule wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameelezea mambo 10 ambayo Rais Dk. John Magufuli, anapaswa kuyafanya ili kuweka misingi ya mabadiliko nchini.
Mbunge Mteule wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameelezea mambo 10 ambayo Rais Dk. John Magufuli, anapaswa kuyafanya ili kuweka misingi ya mabadiliko nchini.
Moja ya mambo ambayo ameandika kwenye waraka wake jana, Zitto
amemshauri Rais Dk. Magufuli kuweka wazi mikataba yote ya rasilimali za
nchi.
"Kuna wakati Thomas Sankara (Rais wa zamani wa Burkinafaso) aliwahi
kusema kwamba huwezi kuleta mabadiliko yoyote ya kweli kwa taifa kama
hutakuwa na kiwango fulani cha wendawazimu,” alisema Zitto kwenye waraka
huo.
Ushauri mwingine wa Zitto ni kwamba Dk. Magufuli afute posho zote
za vikao katika mfumo mzima wa serikali kama mpango wa maendeleo
unavyotaka
Amemshauri pia kufuta viongozi wa serikali na wanasiasa kusafiri
kwa daraja la juu kwenye ndege isipokuwa Rais, Makamu wa Rais na Waziri
Mkuu.
Zitto kwenye waraka huo pia amemshauri Dk. Magufuli kufuta matumizi
ya mashangingi na aliisifu Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwamba
imeonyesha mfano kwenye hilo.
Pia alimshauri Rais Dk. Magufuli afute uagizaji wa sukari kutoka
nje na badala yake ianzishwe miradi ya miwa ili nchi iuze sukari Nje.
Jambo la sita aliloshauri Zitto ni kuweka weka wazi taarifa ya
serikali kuhusu utoroshaji wa fedha na kufungua mashtaka dhidi ya
wahusika mara moja.
Alisema Dk. Magufuli anapaswa kuipa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia
Rushwa (Takukuru) mamlaka ya kukamata na kushtaki na kila mwenye mali
athibitishe mwenyewe ameipataje.
Alisema mali na madeni ya viongozi yawe wazi kwa umma na wananchi waruhusiwe kuhoji.
Katika jambo la tisa, Zitto alimshauri Dk. Magufuli kuruhusu mshindi wa uchaguzi Zanzibar atangazwe na afanye naye kazi.
Zitto katika ushauri wake wa mwisho alimtaka Rais Dk. Magufuli
kuendelea na mchakato wa Katiba kwa kuanzia alipoishia Mwenyekiti wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na kuachana na Katiba
Pendekezwa.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment