Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi
wa dini wakati alipowasili katika kambi ya Rumasi-Lukole iliyopo wilayani
Ngara,mkoani Kagera,kambi hiyo hutumika
kupokea wakimbizi wanaotoka nchini Burundi ambapo baadae hupelekwa katika
makambi ya Nyarugusu yaliyopo mkoani Kigoma.Waziri Mkuu yupo mkoani Kagera kwa
ziara ya kikazi.
Kikundi cha ngoma za kitamaduni cha Umoja, wakicheza
ngoma wakati Waziri Mkuu,Kassim
Majaliwa alipowasili katika kambi ya Rumasi-Lukole iliyopo wilayani
Ngara,mkoani Kagera, kambi hiyo hutumika kupokea wakimbizi wanaotoka nchini
Burundi ambapo baadae hupelekwa katika makambi ya Nyarugusu yaliyopo mkoani
Kigoma.Waziri Mkuu yupo mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi,iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi,Harrison Mseke, akisoma taarifa ya kambi ya Rumasi-Lukole mbele
ya Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu kambini hapo
kukagua kambi hiyo na kuongea na raia wa Tanzania na wakimbizi wa Burundi
wanaoishi kambini hapo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni,akizungumza na wakimbizi wanaoishi katika kambi ya Rumasi-Lukole(hawapo
pichani),wakati ya ziara aliyoongozana na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.Kambi
hiyo iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera hupokea wakimbizi kutoka nchi ya
Burundi kabla ya kuwapeleka kwenye makambi ya wakimbizi ya Nyarugusu,mkoani
Kigoma.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa,akizungumza na raia wa
Tanzania pamoja na wakimbizi wa Burundi
wanaoishi katika kambi ya Rumasi-Lukole(hawapo pichani), Waziri Mkuu
alitembelea kambi hiyo iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera na kuwaasa wakimbizi hao kuishi kwa kufuata
sheria za nchi pasipo kuvunja amani iliyopo nchini.
Raia wa Tanzania pamoja na wakimbizi kutoka nchi ya
Burundi, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa(hayupo pichani),wakati wa
mkutano aliozungumza nao katika kambi ya wakimbizi ya Rumasi-Lukole,iliyopo
wilayani Ngara,mkoani Kigoma.
Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa(wa tatu kushoto),
akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Wakimbizi,iliyopo chini ya Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Harrison Mseke (wapili kulia),wakati akielekea
kukagua mabweni wanayolala wakimbizi kutoka Burundi katika kambi ya
Rumasi-Lukole,iliyoko wilayani Ngara,mkoani Kagera.Wa kwanza kushoto ni Naibu
Waziri wa Nishati na Madini,Dk.Medard Kalemani , wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni na wa kwanza kulia ni mwakilishi wa
Shirika la kuhudumia wakimbizi Duniani(UNHCR),Gerald Ndabimala.
Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa,akikagua mabweni
wanayolala wakimbizi kutoka nchini Burundi katika kambi ya Rumasi-Lukole inayotumika kupokelea wakimbizi
hao.Kambi hiyo iko wilayani Ngara,mkoani Kagera.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara
ya Huduma za Wakimbizi,iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi,Harrison Mseke.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imeandaliwa
na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
0 comments:
Post a Comment