Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu wa
CCM Mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala akiongea na waandishi(ambao hawapo
pichani) juu ya wanachama 25 waliowafuta uanachama kwasababu ya
kukisaliti cha wakati wa uchaguzi mkuu oktoba mwaka jana.
Katibu wa
CCM mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala akielekezana jambo kwenye ilani ya
chama na katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoa Stanely Mkandawile kulia ni
Daniel Gorge Katibu msaidizi kigoma vijijini
Na Editha Karlo,wa blog ya jamii, Kigoma.
CHAMA
cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Kigoma kimewafukuza uanachama 25 wa chama
hicho baada ya kukisaliti chama kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Okt0ba
25 Mwaka jana.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari kwenye ukumbi wa CCM Mkoa Katibu wa CCM
mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala alisema kuwa uamuzi huo wa kuwafuata
uanachama ulitolewa na kikao cha halmashauri kuu cha Mkoa kilichofanyika
tarehe 2 march mwaka huu.
Naomi
alisema kuwa baaada ya uchaguzi mkuu kufanyika chama kilianza
kufanyatathimini na changamoto walizokutana nazo kipinchi cha uchaguzi
mkuu.
''Kwenye
tathimini yetu hiyo tuliweza kugundua kuna baadhi ya wanachama ambao
walikuwa siyo waaminifu kipindi cha uchaguzi mkuu walikuwa wakikisaliti
chama tena wengine walikuwa viongozi na wengine waliogombea ubunge na
kushindwa kwenye kura za maoni tumeamua watupishe sisi tuendelee
kutekeleza ilani ya chama''alisema Kapambala.
Aliwataja
wanachama waliofukuzwa uanachama kuwa ni pamoja Venance Mpologomi,Paul
bahinda, Damasi Shetei,Gidioni Bunyanga,Edger Mkosamali,Pili
Waziri,Pendo Jumanne,Robinson Lembo na Juma matete.
Wengine
waliofukuzwa uanachama ni Idd Lugundanya,Juma Kifuku,Edga
Bisoma,Staphord Kumuhanda,Jenoveva Bisana,Salehe Anatori,Abdallah
Chugu,Atanas Andrea,Bigilimana Vyanda,Jonas Kafyiri,Isack
Braytony,Christopher Chiza,Fanuel Kasogota,Laulent Bikulamuchi,Ibramu
Shikuzilya na Paul Chabandi.
Alisema
wanachama hao walifukuzwa uanachama wa chama cha mapinduzi tayari
wameshahamia vyama vingine pia tathimini ya uchaguzi Mkuu bado
inaendelea.
Naye
Katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Kigoma Staney Mkandawile alisema
kuwa sasa hivi kazi iliyopo ni kutekeleza ilani ya chama na kuumunga
mkono Rais John Magufuli kauli mbiu ya hapa kazi tu.
''Chama
hakitamuonea mtu yeyote,ni bora tubaki wachache ndani ya chama lakini
tuwe tunatekeleza ilani ya chama na kukipenda chama"Alisema Mkandawile
0 comments:
Post a Comment