Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya, (kushoto), akimpatia mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni75 Kaimu mwenyekiti wa Saccos ya Ishimwe Kigoma Bi.Gabriela Hangula wakati wa hafla ya kukabidhi fedha kwa vikudi vya benki za vijijini (VICOBA), mkoani humo,. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. John Ndungulu,
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania, (NEEC),
Bi. Beng’ Issa na Afisa Mtendaji Mkuu, (CEO) wa Benki ya Posta Tanzania,
Bw. Sabasaba Moshingi.Benki ya Posta imekabidhi jumla ya silingi
milioni 175 kwa vikundi hivyo viwili ikiwa ni mpango wa
kuwawezesha wananchi kwa kuwakooesha fedha kuinua mitaji yao chini ya
udhamini wa baraza hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya (kushoto), akimpa mfano wa hundi yenye
thamani ya shilingi milioni 100 Mwenyekiti wa Saccos ya TWCC Kigoma,
Dorothy Takwa. Wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma John
Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi
Tanzania Bi. Beng’ Issa na Afisa Mtendaji wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akishuhudia makabidhiano hayo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akiongea na
wana-saccos wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji, kabla ya kuwakabidhi kiasi cha
fedha Shs milioni 175/=kama mkopo ili kuinua mitaji yao. Kutoka kushoto
ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa
Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Tanzania, (NEEC), Bi. Beng’ Issa
na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya
Mkurugenzi
wa Idara ya Mikopo wa Benki ya Posta Tanzania, Henry Bwogi akimpa
zawadi mmoja wa mwanachama wa Saccos, kulia ni Afisa Uhusiano na
Mawasiliano ya Benki Tanzania, Timotheo Mwakifulefule.
0 comments:
Post a Comment