Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
15/2/2016
Dar es Salaam.
Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetoa tamko kuhusu hali ya wakimbizi nchini
kuanzia mwezi Aprili mwaka 2015 hadi tarehe 10 Februali, 2016.
Akitoa tamko hilo leo jijini Dar es salaam Msemaji wa Wizara hiyo Isaac Nantanga amesema kuwa Serikali imekuwa ikipokea raia toka Burundi wanaoingia nchini Tanzania kutokana na machafuko yaliyotokea nchini humo.
“Kiasi cha wakimbizi 129,210 toka nchini Burundi wameingia nchini kuomba hifadhi kutokana na machafuko yaliyotokea nchini mwao tangu mwezi Aprili mwaka jana hadi sasa” alisema Nantanga.
Nantanga
ameongeza kuwa kati ya wakimbizi 129,210, wakimbizi 79,290
wanahifadhiwa katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu Mkoani Kigoma na
wengine 45,487 wanahifadhiwa katika kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo
Wilayani Kibondo na 4,543 wanahifadhiwa katika kambi ya wakimbizi
Mtendeli iliyopo Wilayani Kakonko.
Ameeleza
kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na wadau wengine imekuwa
ikitoa huduma muhimu kama vile za afya, chakula, maji na ulinzi ili
kuhakikisha wakimbizi wanaishi kwa usalama.
Mbali
na hayo Tanzania inawakimbizi wengine ambao wapo katika kambi ya
Nyarugusu ikijumuisha Wakongo 61,887, Wasomali 150 na wengine 189 toka
katika nchi mbalimbali na kupelekea nchi ya Tanzania kuwa na jumla ya
wakimbizi 191,436 ambao wamehifadhiwa katika makambi.
Wizara
ya Mambo ya Ndani imeendelea kushughulikia Raia wa nchi za nje
walioomba vibali cha kupatiwa hifadhi ya ukimbizi, hivyo maombi 815
yameshashughulikiwa na Kamati ya Kitaifa kuona kama wanastahili kupewa
hadhi ya ukimbizi.
0 comments:
Post a Comment