Kigoma Ujiji ni manisipaa katika Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania na makao makuu ya mkoa huu. Inaunganisha miji ya kihistoria ya Ujiji na Kigoma. Manisipaa hii ilikuwa na wakazi wapatao 215,458 wakati wa sensa 2012.
Kigoma na Ujiji ziko kando la Ziwa Tanganyika katika magharibi ya Tanzania.
Historia
Ujiji ni kati ya miji ya kale zaidi katika Tanzania bara. Ilikuwa kituo kikuu cha njia ya misafara iliyofika hapa kutoka miji ya pwani kama vile Bagamoyo, Saadani au Pangani. Kutoka hapa bidhaa kama pembe za ndovu na watumwa kutoka Kongo na Tanzania bara zilipelekwa tena pwani.
Tangu uenezaji wa ukoloni wa Kijerumani Ujiji ilikuwa pia mahali pa makampuni ya Kizungu na makao makuu ya Mkoa wa Ujiji katika utawala wa koloni
Tangu kufikia kwa meli za kisasa ikaonekana ya kwamba mwambao wa
Ujiji haukufaa sana kwa meli na hivyo mji mpya ulianzishwa kwenye hori
la Kigoma karibu na Ujiji. Mji mpya ya Kigoma ukakua haraka ukawa pia
kituo kikuu cha Reli ya Kati kutoka Dar es Salaam iliyokamilishwa mwaka 1914 miezi michache kabla ya
Mji ulianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani kwenye rasi ndogo inayoingia katika maji ya Ziwa Tanganyika na kuwa na nafasi ya bandari kwa meli za ziwani. Hapa ilikuwa pia mwisho wa Reli ya Kati kutoka Daressalaam.
Baada ya kukamilishwa kwa njia ya reli katia Februari 1914 vipande vya meli mpya Goetzen
vilifika Kigoma kutoka Ujerumani vikaunganishwa hapa. Meli hii
ilizamishwa wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, ikafufushwa tena na
inahudumia mabandari ya Ziwa Tanganyika hadi leo kwa jina la "Liemba".
WIKI PEDIA
0 comments:
Post a Comment