WATOTO sita wakazi wa kijiji cha Mubanga wilaya ya Buhigwe mkoani
Kigoma, wamekufa baada ya kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa
iliyokuwa ikinyesha vijiji jirani na kijiji hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Marko Gaguti akizungumza na gazeti
hili kwa njia ya simu, alisema mauaji hayo yalitokea juzi Jumapili
mchana.
Kanali Gaguti alisema watoto hao ambao walikuwa wanane, walikuwa wakitoka kanisani na wengine wakichunga mifugo ya wazazi wao.
Walikumbwa na mauti hayo baada ya kukumbwa na maji ya mvua iliyokuwa ikinyesha vijiji vingine.
Wakiwa kando ya mto, walikumbwa na dhoruba ya maji ambayo yalikuwa
yakitokea maeneo ya mlimani na yaliwatumbukiza kwenye korongo ambako
watoto wawili walijiokoa kwa kushika majani kando ya mto huo.
Aliwataja waliokufa katika ajali hiyo ya maji kuwa ni Joseph Daniel
(10), Meris John (10), Wence Tryphone (11), Sedekia Philemon (9) huku
akiwataja watoto wengine wawili ambao miili yao haijapatikana kuwa ni
Kaleb Nashon (14) na Habil Gordwin (8).
Mkuu wa Wilaya alisema hadi jana mchana, ambako maziko ya watoto
wanne yalikuwa yakifanyika miili ya watoto wanne ilipatikana na kuzikwa
kwa jitihada za vikosi vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na
wananchi.
CHANZO GAZETI LAHABARI LEO
0 comments:
Post a Comment