Na. Judith Mhina na Lilian Lundo - MAELEZO
Serikali
kupitia Mradi wa Mpango wa Kuboresha Elimu – EQUIP (Education Quality
Improvement Programme) imeendelea kuboresha mfumo wa Elimu hapa nchini
katika nyanja ya mitaala kwa wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la
tatu, uongozi bora katika shule za msingi pamoja na mifumo ya utoaji
taarifa na takwimu sahihi.
Mratibu
wa mradi huo hapa nchini Bw Johan Bentinck, amesema hayo leo jijini,
Dar es Salaam alipokuwa akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo na
namna ambavyo umefanikiwa katika kuboresha Elimu kwa wanafunzi wa shule
za msingi katika mikoa saba hapa nchini.
Mradi
huo umetoa fursa kwa walimu kupata mafunzo ya namna ya ufundishaji bora
utakaomuwezesha mwanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu kujua
kusoma, kuandika na kuhesabu ndani ya muda mfupi na kwa ufasaha.
Aidha
kupitia mradi huo ufundishaji darasa la Kwanza mpaka la Nne umeboreshwa
ambapo mwanafunzi anaweza kuunganisha maneno kwa kutumia sauti. Vile
vile kumekuwepo na njia nyingine za kufundisha kupitia nyimbo na michezo
mbalimbali kwa wanafunzi wa madarasa ya awali.
Pia
mradi umewezesha kuanzishwa kwa madarasa ya awali ambayo hayakuwepo
katika shule za msingi zilizoko vijijini. Wanafunzi wa madarasa hayo
wamekuwa wakifundishwa na walimu wa kujitolea kwa muda wa wiki 12 na
baada ya hapo hujiunga na darasa la Kwanza.
Aidha
mradi huo umeleta mafanikio makubwa katika sekta ya Elimu hapa nchini
ambapo kasi ya ya kutamka maandiko kwa mwanafunzi wa darasa la Kwanza
mpaka la Tatu ilikuwa 21.3 mwaka 2014 na sasa ni 30.0
“Mradi
huo kwa sasa unahusisha mikoa ya Dodoma, Kigoma, Shinyanga, Simiyu,
Tabora, Mara na Lindi huku mikoa mingine miwili ya Katavi na
Singida inategemea kuongezwa mwaka 2017,” alifafanua Bentinck.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment