NA MAGRETH MAGOSSO,KIBONDO.
SHIRIKISHO la Mpira Barani Ulaya (UEFA) kwa kushirikiana na Kampuni ya kutengeneza magari ya Chivrolet ya Marekani imewakabidhi mipira 60 kwa ajili ya Soka la Watoto
walio chini ya miaka 12 kwa shirika la Umoja wa Mataifa UNHCR la
kuhudumia wakimbizi katika Kambi ya Nduta iliyopo wilaya ya Kibondo na
Kakonko kwenye kambi ya Mtendeli zote za Mkoa wa Kigoma .
Akithibitisha hilo juzi Mkuu wa UNHCR Kibondo Dost Yousafzai alisema wamepokea mipira hiyo kwa nia ya kuwaunganisha na
kuthaminiana baina ya watanzania na warundi katika tasnia ya michezo
hususani katika soka la mpira wa miguu kwa watoto waishio kambini kwa
kuwa wafrika wote ni ndugu .
Alisema
pamoja na UEFA na kampuni hiyo kutoa kwa ajili ya kambi hizo,shirika la
UNHCR wametoa mipira 20 kwa ajili ya vijiji vinavyoishi karibu na kambi
ya nduta ya kibondo na mipira 20 kwa vijiji vinavyoishi jirani na kambi
ya mtendeli,ili waratibu wa chama cha mpira wilayani humo wagawe kwa
timu hai ili kuimarisha michezo baina ya raia na wakimbizi.
Akipokea mipira hiyo kwa niaba ya wanakijiji Katibu
wa Chama cha mpira Kibondo James Evalist alisema kwa leo anachukua
mipira 10 tu,na mipira miwili aliikabidhi kwa timu ya Birutana ambayo
inashiriki mashindano ya mechi za ujirani mwema baina ya Burundi na
Tanzania huku mipira 10 ikisalia kwa mkuu wa UNHRC.
’ mipira ya watoto haihimili vishindo kwa timu za wakubwa, siikatai na nawashirikisha wanamichezo wa kibondo lakini kama
mmeamua kutusidia mlete mipira inayokidhi mahitaji ya timu za wakubwa
lakini tunaomba mturekebishie uwanja wa Mpira kwa kuwa uwanja uliopo ni
una kokoto tupu, alisema James.
Naye Kaimu Mkuu wa makazi Kambi ya Nduta Jesca Ntaita alitoa mwito kwa Watanzania
na Warundi wanaoishi katika makambi ya wakimbi kufuata taratibu za nchi
kwa kuwa kuna baadhi ya watanzania huingia makambini kwa vibali vya
warundi na warundi vivyo hivyo.
Na Mtendaji wa kijiji cha Biturana Henry Thomas alisihi shirika la UNHCR kuwa waendeleze mashindano ya ujirani mwema baina ya raia wa pande zote mbili waishio katika kambi hizo,kuwa yasiishie kambini bali yaongeze wigo wa mashindano hayo.
Aidha kudhihirisha kuwa wanaweza kusakata kabumbu timu ya kambi ya mtendeli iliwabugiza goli 4-0 dhidi ya Timu ya kijiji cha Kasanda huku timu ya kambi ya nduta iliwafunga bao 2 Timu ya Kijiji cha Biturana ya wilayani.mwisho.
0 comments:
Post a Comment