Judith Mhina - Maelezo
Wazazi Halmashauri ya Kakonko, wafanikiwa
kutoa chakula katika shule 59
zilizopo katika Halmashauri hiyo kuamzoa mwaka
2015.
Mkoa wa Kigoma una jumla ya Halmashauri 8 na kati ya hizo ni Kakonko peke yake ndio
imefanikiwa kutoa huduma ya uji shuleni. Nikiongea na Waratibu kata kata 5 za Kakonko Bw Jobson Johnston,
Scolastica Andrew, Paschal Mlelema, Eliud Kayigwe na Samson Sike kwa wakati mmoja
wamesema hatukujua kama Halmashauri nyingine hawana huduma hiyo katika shule zao
walidhani ni mpango wa Mkoa
Hata hivyo, walisema:” Changamoto walizoziainisha
waratibu Kata wa Halmashauri nyingine hazina mashiko hivyo ni vema wakajithatiti
kuhamasisha wazazi nina hakika wakielewa
umuhimu wa chakula shuleni , watakubali kuchangia na hatimaye watoto watapata
Uji na kutoa huduma hiyo.
Watoto wa Shule ya Msingi ButaLe Maalum wakipata
Chakula cha Mchana shuleni
Waliongeza kwa kusema utafiti wa Shirika la
Kimataifa la Watoto UNICEF uliofanyika 2001-2003, ulionyesha watoto waliowengi wa shule za
msingi Mkoa wa Kigoma wamedumaa kwa kubeba mizigo mikubwa kuliko uwezo wao na kukosa
chakula bora, wakati Mkoa unakila aina ya chakula, na kuongeza
mafuta ya mawese matunda mbogamboga za majani yote yanayopatikana Tanzania yapo
Kigoma, , hivyo hakuna sababu ya msingi ya
watoto kudumaa.
Mratibu Kata kiongozi wa Kakonko kwenye Warsha
ya Mpango wa Kuinua Kiwango cha Elimu, Bw Jobson Johnston alisema kila mzazi anachangia
kilo 5 ya mahindi, hivyo shule kupata mahindi zaidi ya mahitaji ya mwaka ,
ambapo huuza kiasi kwa ajili ya kupata fedha
ya kununulia maziwa, sukari na mafuta ya mawese.
Uji unaotolewa mashuleni umekuwa na virutubisho
bora kabisa kumfanya mwanafunzi apate usikivu wamasomo darasani, nakuweza kufanya
vizuri.Kila mwanafunzi huja shule na kikombe chake kwa ajili ya huduma ya kupata
uji.
Kakonko in jumla ya kata 13 nazo ni Kiziguzigu, vijiji 3 Gwarama, vijiji 6 Kasuga, vijiji 3
Mugunzu, vijiji 4 Muhange, vijiji 4 Kitanga, vijiji 3 Kasanda, vijiji 7 Nyabibuye,
vijiji 2 Gwanumpu, vijiji 4 Kakonko, vijiji 4 Kanyonza, vijiji 1
Nyamtukuzavijiji 3 na Rugenge vijiji
4 ambapo kwa ujumla kuna shule 59 za Msingi za Serikali.
Halmashauri ya Kakonko ni kati ya Halmashauri
mpya zilizoanzishwa mwaka 2014, ina
jumla ya shule za Msingi 59, ambazo
kwa sasa zote zimeingia kwenye mpango wa kupata chakula shuleni., Aina ya
chakula kinachotolewa ni uji na Baadhi
zinztoa Ugali na maharage aidha, chakula kinapata virutubisho kwa kuwekwa
mafuta ya mawese na zile shule zenye kufuga ngombe wanaweka maziwa kwenye uji hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kupandisha mahudhurio kwa watoto kupenda kwenda shule.
Mkoa wa Kigoma ni kati ya mikoa yenye uzalishaji
mkubwa wa chakula hapa nchini, wenye mazingira mazuri ya kupata mvua bila vikwazo.
Ardhi yake ni nzuri yenye rutuba sehemu nyingi wanalima kilimo hai ,yaani bila kutumia
mbolea za chumvu cnumvi, lakini kupata mavuno mengi. Hakika Mkoa huu hauna sababu
kwa nini usitoe chakula katika shule za Msingi zote Mkoa mzima.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment