Judith Mhina – MAELEZO
Shule za Msingi za Serikali katika Halmashauri ya Buhigwe zipo 88 zamuenzi Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere kwa kutekeleza kwa vitendo miradi 102 ya
Elimu ya Kujitegemea.
Hayo yamesemwa na Waratibu Elimu
Kata 5 wa Halmashauri hiyo,
waliokuwa wakihudhuria Mafunzo ya siku
mbili yaliyoendeshwa na Mpango wa Kuinua Elimu Tanzania EQUIP – TZ, Mwezi Novemba
mwaka huu, katika Ukumbi wa VanCity katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Kigoma.
Kiongozi wa Waratibu Kata hao Mwalimu Maxmillan Joseph alisema:”
Halmashauri ya Buhigwe imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwa na miradi ya elimu ya kujitegemea na
kupunguza dhana ya utegemezi kwa serikali
kwa asilimia mia moja”.
Mwalimu Maxmillan aliongeza :” Mfano zoezi zima la utengenezaji
wa madawati katika Mkoa wa Kigoma, mbao
zilizo nyingi zimetoka katika miradi ya kujitegemea ya Shule za Msingi za
Buhigwe, hili ni jambo la kujivunia.”
Miradi ya shule hizo za Msingi ina lengo la kuwaandaa wahitimu
katika shule hizo kujengewa uwezo wa kujitegemea kuilingana na mazingira ya
mahali walipo na kuanzisha shughuli zao mara baada ya kuhitimu darasa la saba.
Aidha, baadhi ya miradi hiyo inahusu shughuli za Kilimo, Ufugaji,
Misitu, Mazingira, Ufyatuaji na uchomaji matofali na biashara ya vifaa vya
elimu Mfano shule ya Msingi Mwayaya ipo Kata ya Mwayaya ina mradi wa duka la
vifaa vya elimu vya rejareja, Shule ya Gwimbogo
kupanda miche ya mikaratusi robo ekari,
shule ya Kibila mradi wa migomba nusu ekari, Shule ya Manyovu ufugaji wa kuku 30 na mbuzi 3 majike
Kata ya Muhinda
shule ya Ruhuba A robo ekari bustani ya mbogamboga
Ruhuba B, kilimo cha Migomba nusu ekari,
shule ya Nyarubo ina mradi wa
ufugaji mbuzi jike 1, shule Muhinda kuku
10 wa asili, shule ya Kigaraga uboreshaji shamba la kahawa ekari
nusu. Kata ya Buhigwe shule ya Buhigwe mradi wa migomba robo hekari,
shule ya Kavomo shamba la miti robo ekari na shamba la mbegu za majani ya malisho
ya wanyama robo ekari. Shule ya Nyankoronko kilimo cha mahindi nusu ekari, shule ya Mulera migomba nusu ekari, na mananasi robo ekari shule ya Nyamiti kilimo cha
mananasi nusu ekari, shule ya Kafene mananasi nusu ekari.
Shule Kavomo mbogamboga za kupanga kwenye maji yaani saladi na mradi
wa ng’ombe 2 majike wa maziwa shule ya Rusaba upandaji mti 200 robo ekari Rusaba
B upandaji miti ya kahawa 200 robo ekari, shule ya Mpanzigo uendelezaji shamba
la kahawa nusu ekari. Nyarabingo upandaji wamiche ya kahawa 150 robo ekari. Shule ya Kibwiga kilimo cha
migomba ekari shule ya Kiyanga kilimo cha mananasi, nusu ekari shule ya Mikanda
duka la vifaa vya elimu Nyaregano kuku wa mayai
100 shule ya Kilalama ufugaji wa kuku wa asili 40.
Pamoja na miradi yote hiyo ya shule kiwango cha elimu cha
Halmashauri ya Buhigwe kimepanda kutoka nafasi ya 6 ya wilaya mpaka 4. Kama ifuatavyo, Mwaka 2013 ilikuwa nafasi ya 6, 2014 ilikuwa 5, 2015 5 2016
4 ki Mkoa
Itakumbukwa Muasisi wa Taifa hili Marehemu Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere na Azimio la Arusha ambalo lilitoa muongozo wa Elimu ya Kujitegemea.
Katika Awamu ya Mwalimu na dhana ya kujitegemea ilianza kujengwa kwa mtoto
kuanzia shule ya Msingi, Sekondari, Vyuo vya Ufundi, Vyuo Vikuu
na sehemu za kazi kila Afisa au
Mtumishi wa Serikali alitakiwa kuwa mfano katika kufanya mradi au shghuli
yoyote ya kujitegemea ili mradi isijihusishe na matumizi mabaya ya fedha za
umma au ya nafasi yako kazini.
Dhana hii ya Mwalimu Nyerere, iliweza kujenga Taifa la watu wenye
uwezo wa kumudu maisha yao ya kila siku bila kufikiri kuna baba, mama, mjomba
au shangazi wa kukuhudumia kama kijana. Tafiti mbalimbali zinaonyesha Vijana
wengi wa Tanzania hawawezi kubuni, kutafakari muelekeo wa maisha yake binafsi
na kupelekea lawama zote kuiangukia Serikali kwamba haitoi ajira kwa vijana.
Pamoja na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuandaa nafasi nyingi za uongozi kwa
vijana na kuweka mazingira mazuri kwa vijana kujiajiri, bado tatizo ni
kubwa la vijana kupenda kufanya shughuli
ambazi sio endelevu na ambazo haziwezi
kuwajengea uimara wa kumudu maisha yao ya kila siku.
Wilaya ya Buhigwe ni mfano wa kuigwa na Tanzania nzima kwani shule
za Msingi 88 zote zinamiradi ya
kujitengemea, jambo la kusikitisha Mkoa wa Kigoma Halmashauri zote zilizobakia
hazina miradi ya elimu ya kujitegemea kama Buhigwe. Hakika Buhigwe mnastahili
pongezi , ushauri wangu ni vema mkahakikisha Mkoa wa Kigoma wote unakuwa mfano
bora kwa Watanzania kwani ardhi ipo yenye rutuba haihitaji mbolea kutukana na
asili yake ya udongo uliotokana na Volkano na uwepo wa bonde la ufa la Ziwa
Tanganyika. volkano
0 comments:
Post a Comment