Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkaguzi
Mkuu wa Ndani Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe akimhudumia mstaafu wakati
wa zoezi la uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na
Mipango, linalofanyika katika Halmashauri ya Mji wa Kigoma, Mkoani
Kigoma.
Baadhi
ya Wastaafu Mkoani kigoma wakisubiri kuhakiki taarifa zao katika zoezi
la kuhakiki taarifa za wastaafu wanaolipwa na Hazina, linaloendelea
katika mikoa ya Kigoma na Tabora.
Bibi
Lucy Suzereje aliyekuwa mtumishi wa chuo cha maendeleo – Kihinga Mkoani
Kigoma, akiwa ameshika kitambulisho chake cha kustaafu akisubiri
kuhakiki taarifa zake za kustaafu kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma.
Bw.
Jumanne Mtumwa Kiragu (aliyevaa kofia) ambaye alikuwa mtumishi wa
Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Idara ya Magereza akitoa taarifa zake
za kusataafu kwa Mkaguzi wa ndani wakati wa zoezi la kuhakiki taarifa za
wastaafu Mkoani Kigoma.
Mkaguzi
wa ndani wa Manispaa ya kigoma vijijini Bw. Filbert Muhamba (kulia)
akipata maelezo kutoka kwa mstaafu katika zoezi la uhakiki wa taarifa za
wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango, linalofanyika katika
ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma –Ujiji Mkoani Kigoma.
Mwandishi
wa Habari wa TBC Mkoani Kigoma Bw. Dotto Elias (Kulia) akisikiliza
maelezo kutoka kwa baadhi ya wastaafu Mkoani Kigoma mara baada ya
kukamilisha uhakiki wa taarifa zao.
Mkaguzi
Mkuu wa Ndani Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe akiongea na wahandishi wa
Habari akielezea utaratibu unaotumika katika kuhakiki taarifa za
wastaafu katika zoezi la uhakiki unaendelea katika Halmashauri ya
Manispaa ya Kigoma –ujiji.
Mstaafu
Bw. Maganga Patric akiongea na wahandishi wa habari kuhusu zoezi la
uhakiki linaoendelea Mkoani Kigoma katika Halmashauri ya Manispaa ya
Kigoma –Ujiji.
(PICHA ZOTE NA Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango-WFM)
0 comments:
Post a Comment