Home » » HAFLA YA KAMPUNI YA TIGO KUFUTURISHA WATOTO YATIMA KIGOMA

HAFLA YA KAMPUNI YA TIGO KUFUTURISHA WATOTO YATIMA KIGOMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Meneja wa tigo mkoa Tabora Brighton akitoa neno la kuwakaribisha wageni kwa niaba ya Meneja wa tigo mkoa Kigoma wakati wa hafla ya futari ya pamoja baina ya watoto wanaoishi kwenye kituo hicho na uongozi wa tigo ambayo ilienda sambamba na kukabidhi misaada ya vyakula mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 1.2
Mkuu wa wilaya Kigoma Samson Anga (aliyesimama) akizungumza katika hafla ya kutoa misaada na futari ya pamoja kwa watoto yatima na wanaoishi mazingira magumu cha MWOCACHI cha mjini Kigoma iliyoandaliwa na  kampuni ya simu ya mkononi ya tigo
Mkuu wa wilaya Kigoma Samson Anga ( wa pili kulia) na Mkurugenzi wa kanda ya ziwa wa kampuni ya simu ya mkononi ya tigo Gwamaka Mwakilembe (kulia) wakikabidhi kwa uongozi wa kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha MWOCACHI misaada mbalimbali vya vyakula kwa ajili ya kituo hicho misaada ambayo ilienda sambamba na futari ya pamoja baina ya viongozi wa tigo,wadau mbalimbali na watoto hao iliyoongozwa na Mkuu wa wilaya Kigoma.
 Wageni waalikwa na watoto wanaoishi kwenye kituo cha watoto yatima na mazingira magumu cha MWOCACHI cha mjini Kigoma wakishiriki kwenye futari ya pamoja iliyoandaliwa na kampuni ya simu ya mkononi ya tigo kwa watoto hao.

Mkurugenzi wa kanda kanda ya ziwa wa kampuni ya simu ya mkononi ya tigo Gwamaka Mwakilembe (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa tigo Kigoma,viongozi wa kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha MWOCACHI na baadhi ya watoto wa kituo hicho baada ya kukabidhi misaada mbalimbali ya vyakula.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa