Home » » MWENGE WA UHURU KITAIFA WAWASILI MKOANI KIGOMA,YAIBUA MIRADI LUKUKI ILIYOJENGWA CHINI YA KIWANGO

MWENGE WA UHURU KITAIFA WAWASILI MKOANI KIGOMA,YAIBUA MIRADI LUKUKI ILIYOJENGWA CHINI YA KIWANGO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga akikabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwanamvua Mrindoko.


Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

Mwege wa uhuru kitaifa umeanza kutimua vumbi mkoani Kigoma kwa kuibua miradi lukuki iliyojengwa chini ya kiwango katika halmashauri ya wilaya ya uvinza huku kukiwa na hofu ya ufujaji wa fedha za umma katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Kufuatia hali hiyo Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2017 Amour Amour amekataa kuweka mawe ya msingi katika miradi hiyo mitano, inayohusisha ujezi wa nyumba za walimu vyumba vya madarasa na ofisi mbalimbali na kuagiza kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa mhandisi wa ujenzi wa halmashauri hiyo.

Aidha Kiongozi huyo ametoa muda wa siku tatu kwa muhandisi wa halmashauri ya wilaya ya Uvinza na mkandarasi aliyejenga mradi wa nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Nguruka iliyopo katika kata ya nguruka kurekebisha baadhi ya kasoro zilizobainika katika mradi huo kwa kutumia fedha zao .

Maagizo hayo aliyatoa jana mara baada ya kuanza kukagua na Kuzindua Miradi sita ya halmashauri hiyo katika Shule ya Sekondari Nguruka, ambapo katika mradi wa Nyumba za shule hiyo walibaini kuwepo na nyufa katika majengo hayo na matumizi yafedha nyingi katika kukamilika kwa Mradi huo na kumuagiza mkurugenzi kuwasimamia muhandisi wa halmashauri na Mkandarasi wa mradi kufanya marekebisho ndani ya siku tatu na kupelekewa taarifa ya marekebisho hayo.

Hata hivyo Kiongozi huyo aliahirisha zoezi la uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya kijiji cha Malagalasi kata ya Nguluka Wilayani uvinza mkoani kigoma kufuatia jengo hilo kujengwa chini ya kiwango.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa