Home » » DC KIBONDO AUNDA TUME ZA KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HATI ZA UMILIKI ARDHI

DC KIBONDO AUNDA TUME ZA KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA HATI ZA UMILIKI ARDHI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 
WILAYA ya  Kibondo mkoani Kigoma, inayokadiriwa kuwa na wakaazi zaidi ya laki mbili, hadi sasa lakini  ni wananchi 60 tu ndio wanahati za kumiliki ardhi.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya hiyo Louis Burra ameunda tume mbili zitakazo chunguza  idara ya  ardhi na kuchunguza masuala ya Migogoro ya ardhi na kwanini Wilaya hiyo ina hati chache ilikuhakikisha migogoro hiyo inakwisha na Wananchi wanapata hati. Anaandika Rhoda Ezekiel Kigoma.

Akizungumza jana katika kikao cha baraza la madiwani cha kufunga robo ya Mwaka,Mkuu wa Wilaya ya Kibondo  Bura alisema migogoro ya ardhi katika halmashauri hiyo imekuwa ikiongezeka kila siku, na haiwezekani mpaka sasa halmashauri ina hati 60 tuu na Wilaya inazaidi ya wakaazi laki mbili na viwanja havijapimwa.

Alisema atashirikiana na Mkurugenzi kuhakikisha anaunda tume ya uchunguzi itakayo fanya uchunguzi ni kitugani kinasababisha migogoro inaendelea na baada ya uchunguzi watahakikisha Wanawachukulia hatua za Kinidhamu watumishi wote wanaosababisha matatizo hayo.Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

"Suala la migogoro ya ardhi limekuwa kero kwa Wananchi wa Kibondo hatuwezi kuvumilia jambo hili sitakubali suala hili liendelee, tutaangalia kama kunarushwa inaendelea au kama kunaudanganyifu unaendelea tukibaini tutawashughulikia, na hati niwaombe watumishi kwa kushirikiana na Mkurugenzi muhakikishe mnapima viwanja na kuwapatia hati wananchi ilituweze kupata mapato kupitia kodi zitakazo tolewa na Wananchi", alisema Bura.
 
Chanzo Father Kidevu

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa