Home » » JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  


WANAWAKE wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi, ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa. 

Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi.

Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii. Kwa hiyo pamoja na mengine, tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe. 

Pia dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote.

Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama? Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha mafuta kwenye tumbo za kinamama walio wengi. Sababu hizo ni pamoja na;-

Vyakula feki (Junk food), Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi, kutokunywa maji ya kutosha kila siku, kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala, na kukaa masaa mengi kwenye kiti.

Sababu nyingine ni kutokujishughulisha na mazoezi, mfadhaiko (stress), kula wali kila siku, ugali wa sembe, na kula vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (chipsi, maandazi, nk)

JINSI YA KUONDOA MAFUTA HAYO:
Vyakula vinavyoondoa mafuta kwenye tumbo kwa wanawake ni vifuatavyo;-


1. ASALI NA LIMAU
Chukua asali kijiko kikubwa kimoja cha chakula na majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili, changanya hivi viwili ndani ya glasi moja (robo lita) ya maji ya uvuguvugu na unywe yote mara tu ukiamka asubuhi.

Tumia kwa wiki 3 hivi mpaka mwezi mmoja na hutachelewa kuona tofauti.

2. MAJI YA UVUGUVUGU
Kunywa maji ya uvuguvugu kama lita 1 hivi wakati tumbo likiwa tupu hasa asubuhi ukiamka tu. Hii inasaidia kusafisha mwili na kuondoa mafuta yasiyohitajika.


3. NYANYA
Kula nyanya ambazo hazijapikwa pia inasaidia kupunguza tumbo kwa kina mama, hivyo kula kachumbali ya kutosha kila siku ya nyanya peke yake na utaona mabadiliko.


4. TANGAWIZI
Chemsha chai ya tangawizi, ipua na usubiri ipoe kidogo, ongeza asali mbichi kidogo na pilipili manga kidogo ya unga. Pata kikombe kimoja cha chai hii kila siku asubuhi mapema ukiamka tu. Asali inasaidia kuyeyusha mafuta wakati pilipili itauongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.


5. SIKI YA TUFAA
Siki ya tufaa (apple cider vinegar) inasaidia kupunguza njaa na kukufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu. Kunywa kijiko kikubwa kimoja cha siki ya tufaa mara 1 kwa siku kila siku wakati unakula chakula cha usiku. Kazi nyingine ya hii siki ni kuweka sawa damu, sukari mwilini hivyo ni nzuri pia kwa wenye kisukari.


6. MAJANI YA BIZARI
Majani ya bizari husaidia kuondoa sumu na takataka nyingine mwilini kitu ambacho moja kwa moja hupelekea mlundikano mdogo wa mafuta katika tumbo. Kunywa chai ya majani ya bizari kila siku asubuhi, ukikosa majani unaweza kutumia hata unga wake.


8. ILIKI
Iliki hufanya kazi ya kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na ni dawa nzuri sana ya kuondoa sumu na takataka nyingine mwilini. Iliki pia hutumika katika kupunguza uzito. Tengeneza chai yenye iliki kila siku ndani yake, pia ni kiungo karibu kwa vyakula vingi hivyo hakikisha unaiweka katika kila chakula unachopika kwa matokeo mazuri zaidi.


9. MDALASINI
Mdalasini hufanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini. Chukua kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na uweke ndani ya glasi 1 ya maji ya moto na uache kwa dakika 5 hivi. Ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali mbichi ndani yake na ukoroge vizuri, kisha unywe huo mchanganyiko wote asubuhi ukiamka tu.


10. JUISI YA LIMAU
Kunywa maji ya limau au juisi ya limau kila mara kutakusaidia kuondoa mafuta tumboni kwa haraka sana. Ongeza majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili ndani ya glasi 1 ya maji na uongeze punje 1 ya chumvi ya mawe, koroga vizuri na unywe asubuhi ukiamka tu kila siku.


11. KITUNGUU SWAUMU
Ili kupunguza mafuta tumboni katakata vipande vidogo vidogo (chop) punje 3 mpaka 4 za kitunguu swaumu na unywe na maji vikombe viwili asubuhi tu na kisha shushia na glasi moja ya maji yenye limau kidogo kwa mbali. Hii ndiyo njia nzuri kabisa ya asili ya kuondoa mafuta tumboni kwa haraka zaidi.


12. TIKITI MAJI
Tikiti maji lina asilimia 82 za maji kitu kinachofanya tumbo lako kutokuwa na njaa ya kuhitaji chakula. Tikiti maji lina vitamini C ambayo ni muhimu kwa afya bora. Kula tikiti kila siku.


13. MAHARAGE
Kula maharage kila mara kunasaidia kupunguza mafuta katika tumbo. Maharage yana kiasi kingi cha nyuzinyuzi (faiba) kitu kinachosaidia tumbo lako kutojisikia njaa na hivyo itakuwezesha kula chakula kiasi kidogo.

Kadiri unavyokula chakula kichache ndivyo unavyokuwa mbali na uwezekano wa kuzalisha mafuta mengi tumboni.
Basi kula maharage kila siku.


14. TANGO
Tango lina asilimia 96 za maji na asilimia zinazobaki ni nishati. Tumia kachumbali yenye tango ndani yake kila siku au kula tu tango moja kila siku ili kupunguza mafuta tumboni kwa haraka.


15. PARACHICHI
Parachichi ni tunda lingine zuri sana kwa ajili ya kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini. Parachichi ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (faiba). Parachichi huikimbiza mbali njaa na wewe.

Parachichi lina mafuta lakini ni mafuta mazuri (monounsaturated fatty acids) ambayo yenyewe husaidia kuchoma mafuta na hivyo kuondoa mafuta mabaya tumboni kirahisi zaidi.

Kula parachichi 1 kila siku.

*Mwandishi wa makala haya ni Fadhili Paulo, Tabibu wa Tiba Asilia. Kwa ushauri zaidi; WhatsApp +255769142586.
*Itaendelea Alhamisi ijayo kwa njia zaidi za kupunguza mafuta sumu mwilini.
Chanzo:Nipashe

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa