Home » » MAKALA YA SHERIA:AINA MBILI ZA MALI ANAZOSTAHILI MJANE.

MAKALA YA SHERIA:AINA MBILI ZA MALI ANAZOSTAHILI MJANE.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399
 
Na Bashir Yakub.

Maudhui katika makala haya yanatoka katika Sheria ya Ndoa, sura ya 29, iliyofanyiwa marekebisho 2010, pamoja na Sheria ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mirathi,Sura ya 325, R;E 2002. Ziko aina mbili za mali anazostahili mjane.

 Kwanza ni mali inayotokana na machumo ya pamoja yeye na marehemu mme wake . Pili ni urithi anaostashili kupata kama mrithi wa marehemu.

Kwa mfano, mume amefariki. Lakini kabla hajafa huko nyuma walijenga nyumba yeye pamoja na mke wake. Au walinunua kiwanja yeye na mke au gari nk. Mme sasa amefariki na kuacha hizo mali. Katika mali ya namna hii kuna sura mbili.

Sura ya kwanza ni kuwa katika mali hii kuna “share” ya mme na kuna “share “ ya mke. Na “share” ya kila mmoja inatokana na ukweli kuwa kila mmoja kati yao alichangia kupatikana kwa hiyo mali. Kwahiyo kila mmoja ana “share” yake kutokana na kile kiwango alichochangia. Na mchango tulishasema kuwa sio leta ni lete. Hata kazi za nyumbani kama kupika, kufua, kulea watoto nk. nazo ni mchango katka kupatikana kwa mali.

Sura ya pili, ni kuwa kama mume amekufa basi mwanamke kama mke halali anastahili urithi kutoka mali za mumewe. Urithi huu utatoka katika zile mali anazomiliki mumewe yeye kama yeye. Urithi utatoka katika “share” ya mume na si katika “share” nyingine.

Kwahiyo katika mali ileile mjane atakuwa na haki za aina mbili. Haki ya kupata sehemu yake aliyochangia katika kupatikana kwa mali, na haki ya kurithi mali ya mme wake.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa