Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile(Mb) akishirikiana na wananchi wa Kijiji cha Nyanganga
kuchanganya zege kwa ajili ya kuweka ‘rental’ kwa ajili ya madarasa
manne ya Shule ya Kijiji hicho katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi
kujitolea katika kufanya shughuli za maendeleo.
Mtendaji
wa Kjjiji cha Nyanganga Bw.Erick Ruhomola akitoa taarifa ya Mradi wa
ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kijiji chao kwa Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine
Ndugulile(Mb) ambao uliibuliwa, kubainishwa na kutekelezwa wananchi
wenyewe na wananchi kwa takribani.
Mkuu
wa Wilaya ya Uvinza Mhe. Mwanamvua Mrindiko akimshukuru Naibu Waziri
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine
Ndugulile(Mb) kwa kuja kuonesha mfano wa kuamsha ari ya wananchi wa
Uvinza kujitolea katika shughuli za maendeleo yao.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile(Mb) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyanganga
mara baada ya kushiriki zoezi la kuamsha ari katika ujenzi wa Shule ya
Kijiji hicho.
Wananchi
wa Kijiji cha Nyanganga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) mara
baaada ya kushirikiana naye katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi
kufanya kazi katika ujenzi wa vyumba vine vya madarasa ya shule ya
Sekondari ya Kijiji chao.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile(Mb) akikabidhi mifuko 37 ya Saruji kwa ajili ya
kuunga mkono juhudi za wananchi wa Kijiji cha Nyanganga wa kujitolea kwa
nguvu zao kujenga shule ya Sekondari ya Kijiji chao.
Baadhi
ya wananchi wakifanya kazi ya kumwaga ‘rental’ katika ujenzi wa Shule
ya Sekondari ya Kijiji cha Nyanganga kilichopo Wilaya ya Uvinza Mkoani
Kigoma.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile(Mb) akitia saini katika kitabu cha wageni mara
alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwa ajili ya Ziara ya
siku mbili ya kikazi Mkoani hapo.
Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chaote akitoa taarifa ya Mkoa
kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) katika Ziara ya siku mbili ya kikazi ya
Naibu Waziri huyo Mkoani hapo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile(Mb) akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Nyanganga
mara baada ya kuwasili katika kushiriki ujenzi wa madarasa manne ya
Shule ya Kijiji hicho katika kuamsha ari ya wananchi kujitolea katika
kufanya shughuli za maendeleo.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya Uvinza Bw. Lutabola Weja akitoa ufafanuzi wa
jambo wakati wa zoezi la kuamsha ari ya wananchi kujishughulisha katika
shughuli za maendeleo ambapo wanachi wa Kijiji cha Nyanganga wamejitolea
na kujenga vyumba vinne vya madarasa kwa ajili ya shule ya Kijiji chao.
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile(Mb) ameshiriki ujenzi wa Shule ya Kijiji cha
Nyanganga iliyoko kata ya Kazuramimba, wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma
ikiwa ni jitihada za wananchi wa kijiji hicho kuharakisha upatikanaji wa
huduma ya elimu kijijini hapo.
Akiwa
katika Kijiji hicho Naibu Waziri Dkt. Ndugulile ameshiriki zoezi la
kumimina zege kwa ajili ya kufunga ‘rental’ ya vyumba vya madarasa ya
shule hiyo.
Dkt.
Ndugulile amesema lengo la kuwepo ziara hiyo ni kufuatilia utekelezaji
wa Sera ya Maendeleo ya Jamii (1996), na Sera nyingine za Wizara amabzo
zinasisitiza ushiriki wa jamii katika kuibua mahitaji, kupanga, kuamua,
kutekeleza, kufuatilia na utathmini shughuli za miradi ya maendeleo
ikiwemo uboreshaji wa huduma ya miundo mbinu ya kufundishia na
kujifunzia katika maeneo ya mijini na vijijini.
Mhe.
Ndugulile ameongeza kuwa Ili kurejesha ari ya wananchi kushiriki katika
maendeleo yao kuelekea uchumi wa kati na wa viwanda, Wizara imeamua
kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi za
Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuhamasisha
jamii kushiriki na kuchangia shughuli za maendeleo yao kwa kufanya kazi
za bega kwa bega, kuchangia nguvu zao, rasilimali fedha, rasilimali
vifaa na ufundi kwenye utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundo ya
elimu, afya, kilimo, mifugo, barabara na viwanda vidogo vidogo.
“Nimeambiwa
kuwa mradi wenu wa ujenzi wa shule ya sekondari katika kijiji cha
Nyanganga utasaidia kusogeza huduma ya elimu jirani na wananchi, na
nimevutiwa na hamasa mliyonayo katika maendeleo name nimekuja
kushirikiana nanyi kuendeleza ujenzi wa madarasa ya shule kazi amabyo ni
kigezo thabiti cha cha dhamira ya dhati yawananachi wa kijiji hiki
katika kutoa haki ya msingi ya kumwendeleza Mtoto katika ngazi ya kijiji
na jamii kwa ujumla” alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.
Kwa
upande wake Mtendaji wa Kjjiji cha Nyanganga Bw.Erick Ruhomola amesema
kuwa Mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya kijiji uliibuliwa na
kubainishwa na wananchi wenyewe na kutekelezwa na wananchi kwa takribani
asilimia mia moja hadi kufikia hatua ya kumwaga zege kwa ajili ya
‘rental’.
“Tunaishukuru
Serikali kwa kutuona na kuja kutuunga mkono katika jitihada zetu za
kujiletea maendeleo katika kijiji chetu” alisisitiza Bw. Ruhomola.Naye
Mkuu wa Wilaya yaUvinza Mhe. Mwanamvua Mrindiko amemshukuru Naibu
Waziri kwa kuja kuonesha mfano wa kuamsha ari ya wananchi wa Uvinza
kujitolea katika shughuli za maendeleo yao.
“
Hili ni Jambo la kipekee kwa Mhe. Naibu Waziri kutembelea na kushiriki
na wananchi katika ujenzi wa shule hii” alisisitiza Mhe.Mwnanamvua
Ujenzi
wa Shule ya Sekondari ya Kijiji cha Nyanganga kilichopo Wilaya ya
Uvinza Mkoa wa Kigoma itawasaidia watoto wa jamii hiyo kuwa na shule
karibu na makazi yao ambapo hapo awali watoto hao walikuwa wanatembea
umbali wa kilometa 14 kwenda shule ya jirani.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile yupo katika Mkoa wa Kigoma kwa ziara ya siku mbili ya
kikazi kufuatilia utekelezaji wa Sera mbalimbali zinazosimamiwa na
Wizara yake.
0 comments:
Post a Comment