MKUU
wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti akizungumza na
Baadhi ya Watendaji wa Serikali na wananchi kushirikiana katika shughuli
za maendeleo katika ukusanyaji wa mapato na kufanya kazi.
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
MKUU
wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti amewataka
watendaji wa Serikali na wananchi kushirikiana katika shughuli za
maendeleo katika ukusanyaji wa mapato na kufanya kazi.
Lengo ni kuboresha huduma za kijamii katika Wilaya hiyo na kuinua uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.Mwito
huo aliutoa juzi katika chakula cha pamoja na wazee wa Wilaya ya
Buhigwe ,Watumishi wa serikali, viongozi wa dini na chama pamoja na
kuhamasisha shughuli za maendeleo.
Ambapo
aliwataka kila mwananchi mmoja mmoja, kwa makundi na kwa ujumla wao
kuweka mikakati ya pamoja ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya
elimu, afya, miundombinu na jinsi ya kupatikana haki za wazee.
Mkuu
huyo aliwataka watendaji wa Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi
wote ndani ya Wilaya kusaidia jitihada za kusukuma gurudumu la maendeleo
kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato."Lengo
ni kuwezesha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa mafanikio makubwa
ambapo mapato hayo yatasaidia vijiji ambavyo havina zahanati vipate
huduma hiyo kutokana na mapato hayo," amesema.
Aidha
Gaguti aliwataka watendaji wa Serikali kuhakikisha wazee wa Wilaya hiyo
wanapata haki zao kama wengine ikiwa ni pamoja na kupatiwa matibabu
bure, kwakuwa ni sera ya Taifa mzee asisumbuliwe na apatiwe huduma zote
bila malipo.“Nawashukuru
wazee, viongozi wa vya siasa, viongozi wa madhehebu ya dini na
watumishi wote kwa kuonesha moyo wa kusimamia maendeleo yetu na
kuhakikisha tunapata maendeleo kwa kasi."Ni imani yangu kuwa tutashilikiana kwa mambo mengi ili kuweza kuinua uchumi wetu", amesema Gaguti.
Katika
hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilya ya Buhigwe
Anosta Nyamoga alieleza Halmashauri ya Buhigwe inatoa huduma za afya kwa
wazee katika vituo vyake vya kutolea huduma za afya bure kulingana na
sera na miongozo ya Serikali.
Aidha
wazee wanapewa kipaumbele katika matibabu kwa kutibiwa kwanza. Pia
wazee 14,993 wametambuliwa katika wilaya yetu na wazee 1000 watapigwa
picha na kupewa vitambulisho vya matibabu katika kata 5.Upigaji
wa picha na utoaji wa vitambulisho utaendelea katika kata 15 ambazo
bado hazijafikiwa halmashauri imeendelea kuhamasisha jamii ili kuona
umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya wa jamii (CHF).
Nao
baadhi ya wazee wa wilayani Buhigwe, Loleye Ndalibhonye alimpongeza
Mkuu wa Wilaya kwa kuwakumbuka na kuwasaidia katika huduma za kijamii na
kuwasaidia katika kuwapatia huduma ya afya bure.
Amesema
endapo wilaya hiyo ikiongeza vituo vya afya itasaidia wazee hao kupata
huduma kwa urahisi na Wananchi kuweza kupata huduma hiyo na kupunguza
vifo vitokanavyo na ukosefu wa huda.
0 comments:
Post a Comment