Chaga za kisasa za kukaushia dagaa katika mwalo wa Muyobozi, uliyopo katika kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza, Mwalo ambao ulijengwa na Mradi wa kuhifadhi mazingira ya ziwa Victoria LIVEMP , chaga hizo zinatumika na wavuvi kukaushia dagaa.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega na Ujumbe wake wakitoka kukagua gati katika mwalwo wa Muyobozi uliyopo Wilayani uvinza katika kijiji cha Mwakizega ambapo Naibu Waziri Ulega alifanya ziara leo.
Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Uvinza Bw. Haroon Chande akimueleza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega Anayeangalia Chaga kuhusu chaga hizo za kuanikia dagaa zilizojengwa na mradi wa kuhifadhi mazingira wa ziwa Victoria LIVEMP chaga ambazo ameeleza zimekuwa na msaada mkubwa kwa wavuvi wa dagaa wanaotumia mwalo wa Muyobozi uliyobo Wilayani uvinza katika kijiji cha Mwakizega.
Katika Picha katikati Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akipata maelezo kuhusu Mwalo wa Muyowozi toka kwa Afisa Uvuvi wa Wilaya ya uvinza Bw. Haroon Chande, wakati wa ziara yake mwaloni hapo leo.
Wavuvi wakiteketeza wao wenyewe nyavu haramu zilizokamatwa katika oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu katika ziwa Tanganyika Mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega alipofanya ziara katika Mwalo wa Muyobozi Wilayani Uvinza leo
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega kushoto akizungumza na mfanyabiashara wa samaki aliyejulikana kwa jina la Bw. Ntakokola Issa katika Mwalo wa Kibirizi Mjini Kigoma kuhusu usafi wa vifaa maalum na gari la kubebea samaki, gari no T389 AZY linalotumiwa na Mfanyabiashara huyo lilipokuwa linaonekana katika hali ya uchafu, Naibu Waziri Ulega alikagua Mwalo wa Kibirizi uliyopo Mjini Kigoma leo baada ya kumaliza Ziara yake wilayani Uvinza.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Uvinza kwa kuwa na mikakati thabiti ya kupambana na uvuvi haramu na kutatua kwa kiasi kikubwa migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuwekeza kwenye Ranchi za mifugo.
Ulega ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kugagua Mwalo wa Muyobosi uliyopo Wilayani uvinza ambapo alisema jitihada hizo za wilaya zitachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo na serikali kwa ujumla, kwani ina mkakati wa kutenga maeneo ya Ranchi kwa ajili ya wafugaji.
“Nataka niwahakikishie mimi na wizara yangu tutakuwa tayari kuhamia hapa kulisimamia jambo hili mtakapo tenga hayo maeneo ya kufugia, ili kuwaweka tayari wafugaji katika maeneo hayo na huo ndiyo muharobaini wa kwenda kuondoa matatizo ya wakulima na wafugaji katika nchi yetu kwa mipango ya namna hii inawezekana kabisa, hicho ni kipaumbele chetu mimi na waziri wangu Mhe. Luhaga Mpina katika uongozi wetu tutahakikisha kama siyo kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji basi tutaindoa kabisa, kwa kushirikiana vyema na Halmashauri zetu” Alisema Ulega.
Ulega alisisitiza suala la mapambano dhidi ya uvuvi haramu na ulinzi wa Rasilimali za uvuvi na suala zima la ufugaji wa samaki, nakuwaasa kuachana kabisa na utamaduni wa kuagiza samaki kutoka nje ya nchi.
Naibu Waziri Ulega alisema kuwa fedha nyingi zimewekwa katika mwalo huo wa Muyobozi na kuwataka wavuvi katika eneo hilo kuutumia vizuri mwalo huo wenye hadhi ya kimataifa ambapo ameleza kwa mwaka wa fedha uliopita mwalo huo peke yake umechangia kiashi cha shilingi milioni 28 “ Ninaamini kama mtapasimamia vyema mahala hapa patachangia pato la taifa mara nne zaidi ya mwaka jana. Ninyi ndo muwe walinzi wa kwanza wa rasilimali hizi ili nchi yetu iweze kuinuka” Alisisitiza
Awali, akiongea katika ziara hiyo mwenyekiti wa kijji cha Mwakizega ambapo mwalo wa Muhyobozi umejengwa Bw. Jaffari Abdalah, alisema mwalo huo unakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa nipamoja na gati la mwalo huo kuwa na urefu wa mia 20 ambazo ni chache kwa boti kuegesha kupakua na kupakia kabla na baadha ya shuguli za uvuvi , hivyo ameiomba serikali kuongeza urefu wa gati hiyo ili mitumbwi mikubwa na midogo iweze kufanya shughuli za uvuvi vizuri.
Bw. Jaffar pia alisema wavuvi wa Muyobozi wanakabiliana na changamoto ya kukosa elimu kupitia mafunzo yanayoendana na wakati huu wa kisasa katika sekta ys uvuvi.
0 comments:
Post a Comment