Na Rhoda Ezekiel- Malunde1 blog
Watu saba wamefariki dunia katika ajali ya gari aina ya Scania katika Mlima wa Kasagamba kijiji cha Mkongoro barabara ya kutoka Manyovu wilaya ya Kigoma Vijijini kuelekea mkoani Kigoma.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma Maltini Otieno amesema ajali hiyo
imetokea leo Machi 21, 2018 majira ya saa tatu asubuhi.
Amesema
gari aina ya Scania lori yenye namba T741 AAB ilianguka na kusababisha
vifo vya watu saba akiwemo dereva wa gari hiyo aliyefahamika kwa jina
la Siri Hamis (43) mwenyeji wa Singida pamoja na utingo wake
aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Saidi (23) mkazi wa Manyoni.
Kamanda
Otieno amesema katika gari hiyo walikuwa wamebeba mizigo na watu wanne
mmoja mwanamke na wa tatu wanaume ambapo wote walifariki na majina yao
hayakufahamika.
Aidha
amesema ajali hiyo pia imesababisha kifo cha mwanafunzi aliyefahamika
kwa jina la Eliakimu Samsoni (15 )aliyekuwa akitembea kwa miguu kuelekea
shuleni na gari hilo kumgonga akiwa anatembea.
Amesema
chanzo cha ajari hiyo ni dereva kushindwa kuimudu gari kwenye mteremko
mkali na kusababisha gari hiyo kutelemka kwa mwendo mkali na kumshinda
dereva huyo na kusababisha vifo hivyo.
Kamanda Otieno amewaomba
madereva kuzingatia sheria za barabarani na kuhakikisha gari za mizigo
hazibebi abiria ili kunusuru vifo vitokanavyo na ajali na kuhakikisha
wanazingatia alama za barabarani.
Mabaki ya lori baada ya ajali
0 comments:
Post a Comment