BASHE ASEMA RAIS SAMIA HATAKI UTANI KILIMO CHA UMWAGILIAJI

WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amewahakikishia Watanzania kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuleta mapinduzi sekta ya Umwagiliaji, hivyo miradi yote aliyoahidi itatekelezwa.

Waziri Bashe amesisitiza utekelezaji wa miradi hiyo unaofanywa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji si hadithi bali umelenga  kuinua sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji na kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.

Ameitakata Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kujipanga kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo na wananchi wapuuze wanaowalaghai kuuza mashamba.

Waziri Bashe amesema hayo Wakati akizungumza na wadau wa umwagiliaji katika eneo la mradi wa Luiche, ambapo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha utekelezaji  wa mradi huo

“Leo tumefanya uzinduzi wa Mradi mkubwa wa Umwagiliaji katika Bonde la Luiche Wilayani Kigoma katika Mkoa wa Kigoma.Miradi hiyo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 60 itakwenda kunufaisha zaidi ya wakulima 9312 kupitia kilimo cha Umwagiliaji.

Ameongeza kuwa, wizara inamshukuru Rais Dkt.Samia kwani anafanya kwa vitendo na hataki utani katika kilimo cha umwagiliaji.

 “Tunamshukuru sana sana Rais kwa kutoa bilioni 60 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Luiche . Msiuze aridhi yenu ambayo serikali inawekeza fedha zaidi ya bilioni 60 kwa ajili yenu.Mkoa wa Kigoma ni Mlango wa uzalishaji na mlango wa kuhudumia nchi jirani.Serikali inakwenda kujenga  Jengo la ghorofa tatu ambalo litakuwa kitovu cha umwagiliaji katika mkoa wa kigoma na Ghala lenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tanı 4000, Pamoja na mtambo wa kuchakata mpunga”, alisema Waziri Bashe

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa  kufanikisha utekelezaji wa mradi wa Bonde la Luiche, ambao umekuwa ukizungumzwa toka nchi ilipopata Uhuru na kwamba uwekezaji huo mkubwa uliyofanywa na serikali unakwenda kuleta mapinduzi makubwa kiuchumi kwa wananchi wa Kigoma.

Mndolwa pia ametumia fursa hiyo kupokea maagizo ya Waziri wa Kilimo.
“Mradi huu ni mkubwa na utazingatia uwekaji wa miundo mbinu muhimu kama bara bara na itazingatia Kulinda vyanzo vya maji na mazingira”, alisema Mndolwa

Mndolwa pia aliongeza kuwa Tume imepokea maelekezo ya Serikali  kuwa mradi ujumuishe ujenzi wa   Ghala,nyumba ya watumishi Pamoja na Ofisi ya Umwagiliaji

Wakati akiwasilisha Taarifa ya Umwagiliaji kwa Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Umwagiliaji Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Katuta Mustang, amesema Mkoa wa Kigoma Una eneo linalo faa kwa umwagiliaji lenye ukubwa wa Hekta 147,000 na kwamba Mkoa wa Kigoma una jumla ya skimu za umwagiliaji 59 na ni skimu 6 pekee ndizo zilizoendelezwa.

“Mradi wa Ruiche unajumuisha ujenzi wa Skimu kwa gharama ya shilingi Bilioni 40 na ujenzi wa Bwawa lenye ukubwa wa mita za mraba 710,000 kwa gharama ya shilingi  Bilioni 24,na ujenzi wa mifereji yenye urefu wa jumla ya kilomita 100 kutoa maji mashambani;ujenzi wa nyumba mbili za watumishi na usanifu wa jengo la Umwagiliaji Mkoa” alisema Katuta

Nae kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli emahakikishia serikali kuwa serikali itahakikisha ulinzi wa Mradi na Kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Pamoja  na waziri wa kilimo Hussein Bashe kwa kufikisha huduma ya Umwagiliaji katika wilaya ya Kigoma.

Akimkaribisha Waziri wa Kilimo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto Thobias Andengenye, ameishukuru serikali kwa uwekezaji Mkubwa unaofanywa katika Mkoa wa Kigoma, kupitia kilimo cha umwagiliaji.

“Kilimo cha umwagiliaji ni mühimu sana katika kuinua uchumi wa Mkoa wetu wa Kigoma kwani Mkoa wetu una zaidi ya hekta 100 zinazofaa kwa umwagiliaji lakini mpaka sasa ni hekta 9000 tu ndizo zinazo tumika”, amesema Andengenye.

Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Ngenda Shabani Kirumbe,amemshukuru raid Dkt Samia Suluhu Haasan kwa kufanikisha utekelezaji wa Mradi wa Luiche kwani kufanya hivyo kutawezesha kuongezeka kwa mzunguko wa fedha katika mkoa wa Kigoma.

“Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Haasan kwa uwekezaji wa zaidi ya Trilioni 3 katika Mkoa wetu  wa Kigoma na kutupatia Bilioni 60 za utekelezaji wa Mradi wa Umwagiliaji Luiche.Kataeni watu wanao taka kuwarudisha nyuma kwa kuwadanganya kuwa mtapewa fidia kwa ajili ya kupisha ujenzi wa miradi ya miundo mbinu”, alisema Ngenda

Mradi wa Luiche upo katika wilaya ya kigoma, mkoa wa Kigoma. Mradi huu unajumuisha vijiji vya Kamara, Simbo, Kaseke, Nyamori, Msimba, Matiazo pamoja na Kagera. Mradi huu utakuwa na  ya hekta 3000 zitakazomwagiliwa baada ya ujenzi kukamilika. Mradi huu wa Luiche umegawanyika katika mikataba miwili ambayo ni Mkataba wa ujenzi wa bwawa pamoja na mkataba wa ujenzi wa skimu ya umwagiliaji.


DULLA MAKABILA, LINEX WAPAMBA TAMASHA LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Mkali wa Singeli Abdallah Ahmed maarufu Dulla Makabila akiwa jukwaani kutumbuiza katika tamasha hilo la burudani kuelekea uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Kigoma. 
Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva na Singeli,  Sande Mangu almaarufu Linex na Abdallah Ahmed maarufu Dulla Makabila leo Julai 18,2024  wameingiza shangwe kwa wakazi wa Kigoma kwa kutoa burudani kali katika Tamasha la uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. 

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) inataraji juzindua Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Julai 20, 2024 utakaofanyika katika Uwanja wa Kawawa ulipo Ujiji Kigoma na mgeni rasmi akifaraji kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa. 

Wasanii hao waliopanda jukwaani kwa nyakati tofauti kutumbuiza katika tamasha hilo maalum kuelekea uzinduzi wa Ubereshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililokwenda sanjari na utoaji wa Elimu ya Mpiga Kuru kuhusu Uboreshaji wa Daftari. 

Alianza kupanda jukwaani Linex ambaye ni mzaliwa wa Kigoma na ambaye alikuwa uwanja wa nyumbani akiimba baadhi ya nyimbo zake maarufu ukiwepo wimbo maalum wa kuhamasisha watu kujitokeza kuboresha taarifa zao na kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Linex anae tamba kwa sasa na kibao chake cha 'Mahama ya Mapenzi' kabla ya kushika jukwaani alitumbuiza kwa wimbo maarufu aliyeyoimba na wasnii wenzake kutoka Kigoma wa 'Leka dutigite' aliyoimba na kundi lao la Kigoma All Stars akiwa na wasanii wenzake kutoka Kigoma ambao ni Abdu Kiba, Baba Levo, Banana Zorro, Chege, Diamond, Linex, Makomando, Mwasiti, Ommy Dimpoz, Queen Darling, Rachel na mwanasiasa maarufu mzaliwa wa Kigoma Zitto Kabwe

Makabila yeye nae aliimba nyimbo zake kadhaa ikiwepo 'Pita Huku', 'Furahi', 'Hujaulamba', lakini bila kusahau nyimbo za Simba na Yanga ambazo ziliibua shjangwe kubwa jukwaani. 

Makabila atatumbuiza tena siku ya Uzinduzi Julai 20,2024 mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.

Wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Kawawa Kigoma Ujiji walionesha kufurahishwa na burudani hiyo iliyokonga nyoyo zao vilivyo. 

Aidha, Mbali na Dulla Makabila na Sande Linex pia vikundi mbalimbali vya burudani kama Warumba Shauri, Smart Boys , Vijana Rumba, Chama Dansa, Mwandiga One, Waobama. 

Katika Tamasha hilo kundi la Waobama waliibuka washindi katika vikundi vya kucheza dansi vilivyokuwa vikishindanishwa na kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giviness Aswile. 




Vikundi mbalimbali vilivyokuwa vikishindana katika tamasha hilo, vikitoa burudani. 






Katika Tamasha hilo kundi la Waobama waliibuka washindi katika vikundi vya kucheza dansi vilivyokuwa vikishindanishwa na kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giviness Aswile. 



PINDA AMREJESHEA NYUMBA BIBI ALIYOIHANGAIKIA KWA ZAIDI YA MIAKA 10 KIGOMA


 

Na Munir Shemweta, Kigoma

 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amemrejeshea nyumba Bi Leticia Benedict Choma mwenye umri wa zaidi ya miaka 80 mkazi wa Kigoma Ujiji baada ya kuihangaikia kwa zaidi ya miaka 10 bila mafanikio.

 

Bi. Leticia Choma anadaiwa kudhulumiwa nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake Bw. Benedict Choma iliyopo eneo la Mwanga barabara ya Bibi Titi Kigoma Ujiji kama urithi baada ya nyumba hiyo kuuzwa na msimamizi bandia wa mirathi asiyeidhinishwa na mahakama kwa madai ya kutokuwa na haki ya kumiliki nyumba hiyo licha ya  wazazi wake kujenga na yeye kuzaliwa na kuishi hapo kwa miaka yote.

 

Kwa mujibu wa Bw. John Benedict Matata aliyemsimamia Bi. Leticia, mgogoro wa nyumba hiyo ulianza mwaka 2010 pale walipoanza kufuatilia kuhuisha hati ya nyumba hiyo Plot Na 212 Kitalu M mtaa wa Mwanga Kigoma Ujiji yenye namba ya usajili 13176 iliyokwisha muda wake mwaka 1989. kuisha kwa muda wa a hati  hakumkoseshi haki mmiliki ingawa Bi. Leticia amekuwa akizungushwa kwa miaka yote.

 

Amefafanua kuwa, pamoja na juhudi walizofanya ikiwemo kupita taasisi na mamlaka tofauti kutafuta kwa lengo la kutafuta haki lakini hawakuweza kufanikiwa hadi walipopata fursa ya kukutana na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey  Pinda wakati wa ziara ya Makamu wa Rais mkoani Kigoma.

 

Ameeleza kuwa, katika kutafuta suluhu ya suala hilo Mhe Pinda aliwasikiliza kwa makini na baadaye kuitisha kikao cha pamoja kati ya Mwakilishi wa Kamishna wa Ardhi nchini, Msajili wa Hati na Nyaraka mkoa wa Kigoma pamoja na Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa.

 

Bw. Matata ameweka wazi kuwa, kutokana na nyaraka walizokuwa nazo za umiliki wa nyumba yenye mgogoro na maelezo ya Bi. Leticia kuhusiana na sakata hilo pande zote zilikubaliana pasipo shaka kuwa, Bi Leticia Choma ndiye mmiliki halali wa nyumba hiyo.

 

"Baada ya kufuatilia kwa muda mrefu Mwenyezi Mungu amemleta kiongozi Mhe. Pinda, Mungu amzidishie maisha marefu ndiyo tumepata msaada huu leo kuja kumletea malalamiko na namshukuru sana Mheshimiwa’’ alisema Matata.

 

Kwa upande wake Mhe. Geophrey Pinda ameagiza Bibi Leticia Choma kutobughudhiwa na mtu yeyote baada ya kurejeshewa nyumba yake huku akimtaka Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Kigoma kulisimamia suala hilo.

 

‘’Hakuna wa kuingilia tena kuleta shida, huyu bibi asibughudhiwe na wale wote wanaoendesha dhulma kama hii tutakufa nao’’ alisema Mhe. Pinda


 

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS BUHIGWE NA KIGOMA VIJIJINI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kalinzi akiwa ziarani Mkoa wa Kigoma tarehe 09 Julai 2024.


 

MWALIM MKUU KAKONKO AJINYONGA AKIWA OFISINI KWAKE,AANDIKA UJUMBE UNAOMUHUSU MKURUGENZI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Shule ya Sekondari Kakonko wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Peter Rubonya amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba ofisini kwake mapema leo asubuhi.

Akielezea tukio hilo,Mwalim wa zamu wa shule hiyo Isaac Japhet amesema yeye alifika shuleni hapo saa 12:30 asubuhi ili kuwafundisha wanafunzi wa kidato cha nne masomo ya ziada baada ya kufunga shule wiki iliyopita na baada ya kufika aligundua kuwa hana chaki ambapo mkuu huyo wa shule alimpatia chaki mlinzi ili awape wananfunzi.

Amesema baada ya muda,Mratibu elimu kata pamoja na mmoja wa wazazi walifika ofisini hapo wakiwa na shida na mkuu wa shule na baada ya kuelezwa yupo ndani ofisini lakini baada ya kugonga mlango hawakuweza kujibiwa na ndipo wakaamua kufungua mlango na kukuta mwili wa marehemu ukining’inia dalini.

Mwalim Isaac amesema Mwalimu aliyejinyonga alikuwa akifundisha masomo ya Kemia na Fizikia shuleni hapo hawakuwahi kusikia mgogoro wowote wa kifamilia au kijamii, na mkewe ambaye ni mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM),alifika nyumbani kwake juzi akitokea Dodoma.

Kwa upande wa Mlinzi wa Shule hiyo Kajolo Kajabojabo amesema alikutana na Mkuu wa shule mapema asubuhi akiingia ofisini na kumuomba chaki ambazo alipewa na kuziwasilisha kwa walimu.

"Nilimuona kabisa tukasalimiana, nikamuuliza kama anaweza kuwa na chaki, akaingia ofisini akanipatia boksi moja la chaki.Nikachukua na kisha nikampelekea mwalim aliyehizihitaji, alikuwa kwenye hali nzuri tu, lakini baada ya muda ndo tukio hilo likatokea,"amesema Kajoro.

Akizungumza baada ya kufika shuleni hapo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kujua sababu ikiwa marehemu aliacha ujumbe wowote au laa.

"Hatujajua sababu lakini ni muhimu jamii ikajenga utamaduni wa kueleza matatizo ya ndani yanayoyasibu.Hiyo inasaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuepusha madhara kama haya,"amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Otieno amesema baada ya kupekuliwa kwa mwili wa marehemu walikuta karatasi imeandikwa ujumbe kuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Kakonko Lusubiro Mwakabibi asipodhibitiwa ataua wengi.
Chanzo: Kijukuu

WATU SABA WAFARIKI AJALI YA LORI KIGOMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Na Rhoda Ezekiel- Malunde1 blog
Watu saba wamefariki dunia katika ajali ya gari aina ya Scania katika  Mlima wa Kasagamba kijiji cha Mkongoro barabara ya kutoka Manyovu wilaya ya Kigoma Vijijini kuelekea mkoani Kigoma.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma Maltini Otieno amesema ajali hiyo imetokea leo Machi 21, 2018 majira ya saa tatu asubuhi. 

Amesema gari aina ya Scania lori yenye namba T741 AAB  ilianguka na kusababisha vifo vya watu saba akiwemo dereva wa gari hiyo aliyefahamika kwa jina la Siri Hamis (43) mwenyeji wa Singida pamoja na utingo wake aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Saidi (23) mkazi wa Manyoni.
Kamanda Otieno amesema katika gari hiyo walikuwa wamebeba mizigo na watu wanne mmoja mwanamke na wa tatu wanaume ambapo wote walifariki na majina yao hayakufahamika.

Aidha amesema ajali hiyo pia imesababisha kifo cha mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Eliakimu Samsoni (15 )aliyekuwa akitembea kwa miguu kuelekea shuleni na gari hilo kumgonga akiwa anatembea.


Amesema chanzo cha ajari hiyo ni dereva kushindwa kuimudu gari kwenye mteremko mkali na kusababisha gari hiyo kutelemka kwa mwendo mkali na kumshinda dereva huyo na kusababisha vifo hivyo.

Kamanda Otieno amewaomba madereva kuzingatia sheria za barabarani na kuhakikisha gari za mizigo hazibebi abiria ili kunusuru vifo vitokanavyo na ajali na kuhakikisha wanazingatia alama za barabarani.
Mabaki ya lori baada ya ajali 



ULEGA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA KWA MKAKATI MZURI WA KUINUA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Chaga za kisasa za kukaushia dagaa katika mwalo wa Muyobozi, uliyopo katika kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza, Mwalo ambao ulijengwa na Mradi wa kuhifadhi mazingira ya ziwa Victoria LIVEMP , chaga hizo zinatumika na wavuvi kukaushia dagaa.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega na Ujumbe wake wakitoka kukagua gati katika mwalwo wa Muyobozi uliyopo Wilayani uvinza katika kijiji cha Mwakizega ambapo Naibu Waziri Ulega alifanya ziara leo.
Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Uvinza Bw. Haroon Chande akimueleza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega Anayeangalia Chaga kuhusu chaga hizo za kuanikia dagaa zilizojengwa na mradi wa kuhifadhi mazingira wa ziwa Victoria LIVEMP chaga ambazo ameeleza zimekuwa na msaada mkubwa kwa wavuvi wa dagaa wanaotumia mwalo wa Muyobozi uliyobo Wilayani uvinza katika kijiji cha Mwakizega.
 Katika Picha katikati Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akipata maelezo kuhusu Mwalo wa Muyowozi toka kwa Afisa Uvuvi wa Wilaya ya uvinza Bw. Haroon Chande, wakati wa ziara yake mwaloni hapo leo.
 Wavuvi wakiteketeza wao wenyewe nyavu haramu zilizokamatwa katika oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu katika ziwa Tanganyika Mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega alipofanya ziara katika Mwalo wa Muyobozi Wilayani Uvinza leo
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega kushoto akizungumza na mfanyabiashara wa samaki aliyejulikana kwa jina la Bw. Ntakokola Issa katika Mwalo wa Kibirizi Mjini Kigoma kuhusu usafi wa vifaa maalum na gari la kubebea samaki, gari no T389 AZY linalotumiwa na Mfanyabiashara huyo lilipokuwa linaonekana  katika hali ya uchafu, Naibu Waziri Ulega alikagua Mwalo wa Kibirizi uliyopo Mjini Kigoma leo baada ya kumaliza Ziara yake wilayani Uvinza.
 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Uvinza kwa kuwa na mikakati thabiti ya kupambana na uvuvi haramu na kutatua kwa kiasi kikubwa migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuwekeza kwenye Ranchi za mifugo.
Ulega ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kugagua Mwalo wa Muyobosi uliyopo Wilayani uvinza ambapo alisema jitihada hizo za wilaya zitachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo na serikali kwa ujumla, kwani ina mkakati wa kutenga maeneo ya Ranchi kwa ajili ya wafugaji.
“Nataka niwahakikishie mimi na wizara yangu tutakuwa tayari kuhamia hapa kulisimamia jambo hili mtakapo tenga hayo maeneo ya kufugia, ili kuwaweka tayari wafugaji katika maeneo hayo na huo ndiyo muharobaini wa kwenda kuondoa  matatizo ya wakulima na wafugaji katika nchi yetu kwa mipango ya namna hii inawezekana kabisa, hicho ni kipaumbele chetu mimi na waziri wangu Mhe. Luhaga Mpina katika uongozi wetu tutahakikisha kama siyo kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji basi tutaindoa kabisa, kwa kushirikiana vyema na Halmashauri zetu” Alisema Ulega.
Ulega alisisitiza suala la mapambano dhidi ya uvuvi haramu na ulinzi wa Rasilimali za uvuvi na suala zima la ufugaji wa samaki, nakuwaasa kuachana kabisa na utamaduni wa kuagiza samaki kutoka nje ya nchi.
Naibu Waziri Ulega  alisema kuwa fedha nyingi zimewekwa katika mwalo huo wa Muyobozi na kuwataka wavuvi katika eneo hilo kuutumia vizuri mwalo huo wenye hadhi ya kimataifa ambapo ameleza kwa mwaka wa fedha uliopita mwalo huo peke yake umechangia kiashi cha shilingi milioni 28 “ Ninaamini kama mtapasimamia vyema mahala hapa patachangia pato la taifa mara nne zaidi ya mwaka jana. Ninyi ndo muwe walinzi wa kwanza wa rasilimali hizi ili nchi yetu iweze kuinuka” Alisisitiza
Awali, akiongea katika ziara hiyo mwenyekiti wa kijji cha Mwakizega ambapo mwalo wa Muhyobozi umejengwa Bw. Jaffari Abdalah, alisema mwalo huo unakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa nipamoja na gati la mwalo huo kuwa na urefu wa mia 20 ambazo ni chache kwa boti kuegesha kupakua na kupakia kabla na baadha ya shuguli za uvuvi , hivyo ameiomba serikali kuongeza urefu wa gati hiyo ili mitumbwi mikubwa na midogo iweze kufanya shughuli za uvuvi vizuri.
Bw. Jaffar pia alisema wavuvi wa Muyobozi wanakabiliana na changamoto ya kukosa elimu kupitia mafunzo yanayoendana na wakati huu wa kisasa katika sekta ys uvuvi.
 

WATENDAJI WA SERIKALI,WANANCHI WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA KULETA MAENDELEO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 MKUU wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti akizungumza na Baadhi ya Watendaji wa Serikali na wananchi kushirikiana katika shughuli za maendeleo katika ukusanyaji wa mapato na kufanya kazi.
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kanali Marco Gaguti amewataka watendaji wa Serikali na wananchi kushirikiana katika shughuli za maendeleo katika ukusanyaji wa mapato na kufanya kazi.
Lengo ni kuboresha huduma za kijamii katika Wilaya hiyo na kuinua uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.Mwito huo aliutoa juzi katika chakula cha pamoja na wazee wa Wilaya ya Buhigwe ,Watumishi wa serikali, viongozi wa dini na chama pamoja na kuhamasisha shughuli za maendeleo.
Ambapo aliwataka kila mwananchi mmoja mmoja, kwa makundi na kwa ujumla wao kuweka mikakati ya pamoja ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya elimu, afya, miundombinu na jinsi ya kupatikana haki za wazee.
Mkuu huyo aliwataka watendaji wa Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi wote ndani ya Wilaya kusaidia jitihada za kusukuma gurudumu la maendeleo kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato."Lengo ni kuwezesha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa mafanikio makubwa ambapo mapato hayo yatasaidia vijiji ambavyo havina zahanati vipate huduma hiyo kutokana na mapato hayo," amesema.
Aidha Gaguti aliwataka watendaji wa Serikali kuhakikisha wazee wa Wilaya hiyo wanapata haki zao kama wengine ikiwa ni pamoja na kupatiwa matibabu bure, kwakuwa ni sera ya Taifa mzee asisumbuliwe na apatiwe huduma zote bila malipo.“Nawashukuru wazee, viongozi wa vya siasa, viongozi wa madhehebu ya dini na watumishi wote kwa kuonesha moyo wa kusimamia maendeleo yetu na kuhakikisha tunapata maendeleo kwa kasi."Ni imani yangu kuwa tutashilikiana kwa mambo mengi ili kuweza kuinua uchumi wetu", amesema Gaguti.
Katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilya ya Buhigwe Anosta Nyamoga alieleza Halmashauri ya Buhigwe inatoa huduma za afya kwa wazee katika vituo vyake vya kutolea huduma za afya bure kulingana na sera na miongozo ya Serikali.
Aidha wazee wanapewa kipaumbele katika matibabu kwa kutibiwa kwanza. Pia wazee 14,993 wametambuliwa katika wilaya yetu na wazee 1000 watapigwa picha na kupewa vitambulisho vya matibabu katika kata 5.Upigaji wa picha na utoaji wa vitambulisho utaendelea katika kata 15 ambazo bado hazijafikiwa halmashauri imeendelea kuhamasisha jamii ili kuona umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya wa jamii (CHF). 
Nao baadhi ya wazee wa wilayani Buhigwe, Loleye Ndalibhonye alimpongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuwakumbuka na kuwasaidia katika huduma za kijamii na kuwasaidia katika kuwapatia huduma ya afya bure.
Amesema endapo wilaya hiyo ikiongeza vituo vya afya itasaidia wazee hao kupata huduma kwa urahisi na Wananchi kuweza kupata huduma hiyo na kupunguza vifo vitokanavyo na ukosefu wa huda.
 

KATIBU MKUU WA MIFUGO KUKABIDHI RASMI TAARIFA YA CHAPA YA MIFUGO LEO KWA WAZIRI MPINA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo (mwenye skafu) akiongea na wafugaji kuhusu upigaji chapa mifugo kwenye Kijiji cha Makere Mkoani Kigoma.Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. (Picha na Ngailo Ndatta) 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo akishiriki zoezi la Upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. (Picha na Ngailo Ndatta
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo(mwenye skafu) akiongea na baadhi ya wafugaji kuhamasisha upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. (Picha na Ngailo Ndatta) 
Dereva wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bwana Athuman Ramadhani akishiriki katika zoezi la upigaji chapa katika Mkoa wa Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31. (Picha na Ngailo Ndatta) 

Na John Mapepele, Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo amewataka Wakuu Wote wa Idara katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kwamba timu zote zilizosambaa kote nchini ziwe zimewasili mjini Dodoma leo na kwamba ifikapo saa kumi na mbili jioni ziwe zimewasilisha taarifa kuhusu zoezi hilo kwake ili akabidhi rasmi kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina kwa ajili ya hatua zaidi baada ya zoezi hilo kuisha rasmi leo.

“Wakuu Wote wa Idara,Mhe Waziri anataka Timu za Chapa zirudi Dodoma.Leo saa 12 jioni apate taarifa ya mwisho ya upigaji chapa. Mkurugenzi wa Mipango ratibu timu ya kukamilisha taarifa ” alisisitiza Mashingo kwenye taarifa yake aliyoitoa jana kwa Wakuu wa Idara.

Aidha amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha wamemaliza zoezi la kupiga chapa mifugo yao yote katika muda wa nyongeza uliotolewa na Serikali ambao uliamuliwa kuwa Januari 31mwaka huu.

Akizungumza katika siku za mwisho wakati anahitimisha ukaguzi na uhamasishaji wa zoezi la kupiga chapa katika Mkoa wa Kigoma, Dkt. Mashingo amewaonya baadhi ya wafugaji kutojiingiza katika matatizo ya kupiga chapa mifugo ambayo inatoka nje ya nchi ambapo amesema wakibainika watachukuliwa hatua kali.

Aidha, Dkt. Mashingo amewataka wafugaji wote wasio raia wa Tanzania waliyoingia katika mikoa ya mipakani kuondoa mifugo yao mara moja kwa kuwa haitapigwa chapa badala yake watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Katika hatua nyingine Dkt. Mashingo ambaye pia ni mtaalam bobezi katika eneo la malisho ya mifugo amesema kufanikiwa kwa zoezi la kupiga chapa kutasaidia usimamizi wa Sekta ya Mifugo hapa nchini ambapo alisema awali inakadiliwa kwamba 30% ya malisho yote nchini yalikuwa yakitumiwa na mifugo toka nje ya nchi.

Ameutaka Uongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kutopingana na Serikali badala yake kuongeza ushirikiano na kuwaelimisha wenzao kufuga kisasa ili kuondoa migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

Awali Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina wakati akihitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo kitaifa lililofanyika katika wilayani Itilima mkoani Simiyu, Desemba 31mwaka jana aliongeza siku 30 kwa halmashauri zote nchini ili kukamilisha zoezi la kupigaji chapa mifugo huku akiwavua nyadhifa maafisa wawili wa Wizara kwa kushindwa kusimamia zoezi hilo kikamilifu na wengine wawili wakipewa onyo kali.

Alida kuwa licha ya kuwepo kwa baadhi ya changamoto zilizosababisha zoezi hilo kufanyika kwa asilimia 38.5 tu kwa nchi nzima baadhi ya watendaji wa serikali na viongozi walichangia kulikwamisha ambapo Halimashauri ambazo zikamilisha zoezi la chapa chini ya asilimia 10 zilipelekwa majina ya watendaji wao kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu.

Siku kumi na tano baada ya muda wa nyongeza wa siku thelathini, Mhe. Mpina alitoa tathmini mbele ya Waandishi wa Habari mjini Dodoma, kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa mifugo ambapo Mpina alisema hadi kufikia siku hiyo ya Januari 16 mwaka huu jumla ya ng’ombe 10,306,359 sawa na asilimia 59.3 ya lengo walishapigwa chapa ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ya tathmini ya awali iliyofanywa Desemba 31 Mwaka jana .

Aidha alisema wafugaji wote nchini watakaoshindwa kupiga chapa mifugo yao ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4 kifungu cha 26.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa