Home » » HALMASHAURI KUU YA CCM KIGOMA YAWATIMUA VIONGOZI WAKE WA WILAYA YA KIBONDO

HALMASHAURI KUU YA CCM KIGOMA YAWATIMUA VIONGOZI WAKE WA WILAYA YA KIBONDO


Na Johnson Matinde wa Kigoma yetu


Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCMo)mkoa wa Kigoma imewavua uongozi viongozi wawili wa wilaya ya Kibondo kwa makosa ya kukisaliti chama
Kulingana na barua iliyosainiwa na katibu mkuu wa chama hicho mkoani Kigoma Mohamed Nyawenga maamuzi hayo mazito yamefanyika katika kikao cha halmashauri hiyo kilichofanyika Juni 23 mwaka huu
Waliovuliwa nyadhifa zao ni katibu wa uchumi na fedha wa wilaya hiyo Pascal Katabizi na katibu mwenezi wa wilaya Anselm Batabalo ambao wanadaiwa kushirikiana na viongozi wa vyama vya upinzani kuwachochea madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo kumkataa mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa kisingizio cha kutekeleza maagizo ya viongozi wa juu
Kutokana na makosa hayo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kibondo Majaliwa Lusizi amelazimika kujiuzulu mbele ya kikao hicho nafasi yake kukiongoza chama wilayani humo
Aidha halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Kigoma imemuondoa mkoani humo katibu wa CCM wilaya ya Kigoma Kisali Elia kwa madai kuwa alishindwa kuwashauri vyema viongozi hao kulingana na kanuni za utendaji za CCM
Pia anadaiwa kushindwa kuzima na kutoa taarifa za uasi huo kwa ngazi za juu za chama na kushiriki njama za kukiasi chama jambo ambalo limesababisha CCM ipokwe uenyekiti wa halmashauri ya wilaya kwa kujiuzulu kwa mwenyekiti na kudhalilika kwa jamii
Makosa mengine yaliyotajwa kusababisha viongozi hao kuondoka kuondoka kwenye chama wilayani humo ni pamoja na kutotaka kutumia utaratibu wa chama cha mapinduzi wa kushughulikia matatizo ya kimaadili ya viongozi yaliyokuwa yakimkabili mwenyekiti huo wa halmashauri kupitia vikao vya chama cha mapinduzi.
Kinyume chake wao walitumia njia ya mkato nje ya chama ambayo ni jukwaa la wafanyabiashara kumshinikiza mwenyekiti huyo kujiuzulu
Maamuzi hayo ya halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Kigoma pia yameongezewa nguvu  na hali ya halmashauri hiyo kutoridhishwa na mienendo ya viongozi hao ambapo inadaiwa kuwa kw a muda mrefu utendaji wao umekuwa ukitiliwa mashaka makubwa hadi kufikia hatua ya kuhatarisha uhai wa CCM wilayani humo
Viongozi hao wanadaiwa kuwa mara nyingi wamekuwa wakiegemea mno katika kusaidia upinzani ikiwa ni pamoja na kuthubutu hata kushirikiana nao kwa karibu katika masuala ya mbali mbali kinyume na katiba, kanuni na miiko ya chama
Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Kigoma imesema inatoa adhabu kali kwa viongozi hao baada ya kujiridhisha kwa ushahidi mbali mbali kuwa wamekisaliti chama kwa kiwango kisichoweza kuvumilika, hasa kwa kuthubutu kushirikiana na madiwani wa upinzani na wafanyabiashara wa Kibondo kumkataa mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa CCM.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa