Home » » WATATU WAFARIKI KWA KUPIGWA NA RADI

WATATU WAFARIKI KWA KUPIGWA NA RADI


Na Emma J Matinde Kigoma yetu
KIGOMA
Thursday June 28, 2012

Watu watatu wakiwemo wawili wa familia moja wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti ya kupigwa na radi yaliyotokea siku moja huko wilayani Kasulu mkoani Kigoma
Kamanda wa polisi mkoani Kigoma kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Frasser Kashai amesema tukio hilo limetokea Juni 26 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi katika vijiji vya Rusesa na Kagerankanda wilayani Kasulu.
Amewataja waliofariki katika tukio la kwanza kuwa ni Jackline Leonard mwenye umri wa miaka 12 mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Rusesa na Maria Leonard mwenye umri wa miaka 15 mkulima wote wakazi wa Rusesa wilayani Kasulu.
Amesema tukio limetokea wakati wakiwa njiani kutoka shambani kurejea nyumbani kwao kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha na walifariki muda mfupi baada ya kufikishwa katika zahanati ya Rusesa kwa ajili ya matibabu
Aidha kamanda Kashai amesema katika tukio la pili lililotokea Juni 26 majira ya saa saba mchana huko kijiji cha Kagerankanda Zuwena Cosmas mwenye umri wa miaka 13 mwanafunzi wa shule ya msingi Nyangaza na mkazi wa Kagerankanda alifariki dunia baada ya kupigwa na radi kufuatia mvua iliyokuwa ikinyesha
Amesema katika tukio hilo Rahel Lucas mwenye umri wa miaka 10 mkazi wa kijiji cha Kagerankanda alijeruhiwa sehemu mbali mbali za mwili wake na kulazwa katika zahanati ya Kagerankanda kwa matibabu.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kigoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa